Kocha Rashid Mahadhi amefariki dunia ikiwa ni muda mfupi baada ya timu yake ya Abajalo kupoteza mechi

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971

Rashid Mahadhi amefariki dunia ikiwa ni muda mfupi baada ya timu yake ya Abajalo kupoteza mechi dhidi ya Changanyikeni

Mechi hiyo ilichezwa kwenye Uwanja wa Tandika jijini Dar es Salaam na Abajalo kutoka Sinza maarufu kama Mnyama ikapoteza kwa mabao 3-0. Baada ya kipigo hicho, Mahadhi aliangua kilio akisema wachezaji hawakuonyesha juhudi na wakati mwingine alionekana kutofurahishwa na maamuzi.

Baadhi ya watu wa Ajabalo walilazimika kumtoa eneo hilo la uwanja na kumuingiza vyumbani huku akiendelea kulia. Lakini baadaye ilielezwa, hali yake ilizidi kuwa mbaya baada ya presha kupanda, akaanguka juhudi zilifanyika kumkimbiza hospitali, lakini baadaye alifariki dunia.

Mahadhi alikuwa akimsaidia Kocha Abdallah Kibadeni ambaye kila alipopata nafasi alikwenda kutoa ujuzi wake kwa timu hiyo ya mtaani kwao. Abajalo ni timu ya mtaani kwa Kibadeni na Mahadhi ambao walikuwa wanaishi nyumba jirani Sinza kabla ya kuhama.

Mahadhi ambaye ni mtoto wa nyota wa zamani wa soka, pia ni kaka wa kiungo wa zamani wa Yanga, Waziri Mahadhi 'Mendieta'.

Kiungo huyo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, amesema msiba wa Rashid aliyewika miaka ya 1990 katika Ligi Kuu ya Bara, upo nyumbani kwake, Kimara Bonyokwa na mwili wa marehemu utasafirishwa mapema kesho kwa mazishi kwenye makaburi ya Mnyangani, Tanga.

Waziri amesema marehemu ambaye alipatwa na ugonjwa wa kiharusi kwa zaidi ya mwaka sasa, ameacha mke, Jazira na mtoto, Mahadhi mwenye umri wa miaka 18 sasa. Mungu aipumzishe kwa amani roho ya marehemu. Amina

CHANZO: EATV
 
Chanzo cha kifo ni kiharusi,pressure au mshituko wa matokeo ya mechi?
 
'changanyikeni' wameua bila kukusudia.
 
Rashid Mahadhi amefariki dunia ikiwa ni muda mfupi baada ya timu yake ya Abajalo kupoteza mechi dhidi ya Changanyikeni.

Mechi hiyo ilichezwa kwenye Uwanja wa Tandika jijini Dar es Salaam na Abajalo kutoka Sinza maarufu kama Mnyama ikapoteza kwa mabao 3-0. Baada ya kipigo hicho, Mahadhi aliangua kilio akisema wachezaji hawakuonyesha juhudi na wakati mwingine alionekana kutofurahishwa na maamuzi.

Baadhi ya watu wa Ajabalo walilazimika kumtoa eneo hilo la uwanja na kumuingiza vyumbani huku akiendelea kulia. Lakini baadaye ilielezwa, hali yake ilizidi kuwa mbaya baada ya presha kupanda, akaanguka juhudi zilifanyika kumkimbiza hospitali, lakini baadaye alifariki dunia.

Mahadhi alikuwa akimsaidia Kocha Abdallah Kibadeni ambaye kila alipopata nafasi alikwenda kutoa ujuzi wake kwa timu hiyo ya mtaani kwao. Abajalo ni timu ya mtaani kwa Kibadeni na Mahadhi ambao walikuwa wanaishi nyumba jirani Sinza kabla ya kuhama.

Mahadhi ambaye ni mtoto wa nyota wa zamani wa soka, pia ni kaka wa kiungo wa zamani wa Yanga, Waziri Mahadhi 'Mendieta'.

Kiungo huyo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, amesema msiba wa Rashid aliyewika miaka ya 1990 katika Ligi Kuu ya Bara, upo nyumbani kwake, Kimara Bonyokwa na mwili wa marehemu utasafirishwa mapema kesho kwa mazishi kwenye makaburi ya Mnyangani, Tanga.

Waziri amesema marehemu ambaye alipatwa na ugonjwa wa kiharusi kwa zaidi ya mwaka sasa, ameacha mke, Jazira na mtoto, Mahadhi mwenye umri wa miaka 18 sasa. Mungu aipumzishe kwa amani roho ya marehemu. Amina

Chanzo: EATV
 
Wenger Sugu Jamani Hata Afungwe Ngapi, Hata Hashtuki
Weeee,kuna siku alidondoka kituo cha treni baada ya kuchapwa na Liverpool
 
Mpira ni Mchezo mzuri sana. lakini ukiupenda sana mwisho wake huwa ni matatizo. Ukiwaangalia sana hawa wanaobashiri soka (betting) kwa jicho la huruma ni watu waliochakaa sana na hawapo sawa kiakili kabisa ni kama watumwa wanaohangaika na wamekuwa wavivu kabisa.
 
Siamini kama kichapo cha goli 3-0 kitaondoka na maisha ya MTU ambae amewahi hata kuucheza Mpira mwenyewe professionally na hata kuwa na taaluma ya ukocha, na zaidi akifanya kazi na Abdallah King Kibadeni, . Katika maisha yao ya kisoka, ni Mara ngapi wamefungwa goli kama hizo? Au zaidi ya hizo? Kwa nini asife toka miaka hiyo? Kwa nini afe kwenye mechi ya mchangani isiyokuwa na ubingwa wala fedha yeyote? Tajeni sababu nyingi be ya kifo chake lakini si kipigo cha goli 3. Labda hiyo hypertension inakubalika but not goli 3. Innah lillahi wainnah illahi rajiuni
 
Hakika cc ni wa Mwenyezi Mungu na kwake yeye ndio marejeo yetu___
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…