Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Baada ya kufanya mazoezi na kikosi kwa siku mbili katika kambi waliyoweka nchini Dubai Kocha Mkuu Oliveira Roberto ‘Robertinho’ amejiridhisha kuwa anahitaji mshambuliaji mwingine.
🔹 Robertinho amesema kikosi chake kina washambuliaji wazuri huku akimwagia sifa Nahodha John Bocco lakini ameweka wazi kuwa ili atimize malengo yake anahitaji mshambuliaji mwingine wa kusaidiana na waliopo.
🗣️“Aina ya mshambuliaji ninayemtaka ni mwenye nguvu, kasi na maarifa ya kufunga,” amesema Roberthinho baada ya kumaliza mazoezi ya leo asubuhi.