Ni kweli ila mimi ninakikubali kile cha mwaka 1992/1993,kulikuwa na beki moja anacheza namba mbili nimemsahau,Twaha Hamidu,Edward Chumila,Malota Soma...eeeh bwana ilikuwa SIMBA Kweli,siku walicheza na Atletico Eviacao ya Angola tulishinda goli 3 lakini nahisi Simba haijawahi cheza mechi ngumu zaidi ya ile tena hadi sasa.Atletico kulikuwa na kipa wao anaitwa kanka wemba,mshambiliaji Abilio na wngine wakali acha
Full Kosi Lenyewe lilikuwa kama ifuatavyo;
1. Mohamed Mwameja
2. Kasongo Athuman Mgaya
3. Twaha Hamidu
4. Godwin Aswile Mlimba
5. George Magere Masatu
6. Leny Ramadhani
7. Abdul Mashine
8. Hussein Amaan Marsha
9. Edward Chumila
10. Malota Soma 'Ball Jugler'
11. Uncle Tom Kipese
Siku yenyewe tukiwa bado wadogo, tulichaji betri pale kijijini petu kwa kuzianika juani kwenye kichanja. Tukavizia baada ya taarifa ya habari kutoka RTD wanajiunga na uwanja wa taifa na wakati huo hiyo aviacoa ilikuwa kwenye kiwango cha juu kupita maelezo. Simba ktk ubora wake huwa haishindwi kitu.