Kocha Stars afanyie kazi mapungufu yaliyojitokeza otherwise tumejitahidi sana

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Kulalamika imekuwa tabia yetu watanzania, jana Stars ilicheza vzr sana, hasa Haji Mnoga, huyu kijana wakati anakuja awali akicheza beki ya kulia hatukuwa tukimwelewa kabisa lkn ss hv yuko timamu mno, amekuwa na confidence ya kutosha, jana he was man of the match. KIKOSI Kilicheza vzr mno na kama sio mapungufu ya golikipa kufungwa bao rahisi la kwanza gemu ile tungeweza kumaliza vizuri, ni ukweli kabisa wachezaji wanaocheza nje wameleta mabadiliko makubwa kikosini, Stars inacheza mpira unaonekana, kufungwa ni kawaida tu mbona Brazil jana kafungwa na Argentina nyumbani kwao?

Suala kuwa kwann Manula hakupangwa sijui kwann Kibu kaanza mara kwann Feitoto hakucheza ni mambo ya kijinga tu, kocha ndiye anayejua, sababu kuwa eti kocha ni mwarabu kwahiyo amewabeba waarabu wenzie ni ujinga wa kiwango cha chuo kikuu.

Vijana walikuwa wanapiga pasi za uhakika, walijiamini na kucheza kwa bidii kwa ukubwa sana, Morocco sio wenzetu, kuifunga Morroco ilikuwa ni kudanganyana, tumepunguza sana mabao jana, Watu wamecheza nusu fainal kombe la dunia halafu sisi tuko kwenye take off stage tuwafunge, kweli? Hatuoni hata aibu.

Nampongeza sana kocha, Stars sio mnyonge sasa hv, tulienda kumpiga Niger kwao na wao wamempiga Zambia kwao, hamuoni we deserve respect. Tuwatie moyo wachezaji na viongozi ili tumalize safari vzr, kutukana, kukashifu, kukebehi, kuponda na kujifanya tunajua mpira Sanaa wakati hatukuusomea ni kuudhalilisja mpira, kwenye mapungufu tutoe maoni ili yafanyiwe kazi.

Mwisho, Haji Mnoga amebadilika sana, ana uwezo mkubwa sana akicheza kiungo kuliko beki wa kulia.Jana aliwabana sana waarabu, yeye na Bajana walistahili pongezi kwa mchezo mzuri wa jana.
 
Mimi nampongeza sana huyu kocha ni mjanja sana yeye akikupanga leo kesho hakupangi na siku akikupanga lazima utajituma sana ili uwe unapangwa, huoni samata na msuva walovoingia kama sub wamejituma sana pia muangalie kibu alivokua anakaba na kuwapokonya mipira mabeki wa morocco,

Hspo siku mzize akiitwa atapambana kwa jasho na damu maana kuna kushindani mkubwa
 
Shida kubwa team haina muunganiko yaani wanabutua butua tu.
 
Hayo ni makosa kwa timu sio faida .
Alishindwa nini kubaki na kikosi kilichoanza na Niger au kilichoanza na Algeria .
Bado hana uhakika na mpango kazi wake anajaribujaribu huku akiwa Hana uhakika .

Na katika wachezaji wa nje aliyeleta mchango ni Charles mombwa tu .

Usishangae mechi ijayo akaja na kikosi kipya kabisa
 
Watajijua huko hata wakipigwa 10 sijali
 
Jana almanusra nmpige Ngumi shabiki moja maandazi
Yani mtu anataka stars Im outplay Morocco
 
Hivi kauli ya kujitahidi mnaielewa kweli maana yake???

yaani kafungwa halafu mnasema kajitahidi??? Asingejitahidi alitakiwa apate matokeo gani?

Matokeo ni WIN, DRAW or LOSE. Sasa kama LOSE ni kujitahidi, angedraw au kushinda tungesemaje?

Naona unabwatabwata.. unaongea sana utadhani vile dogo umedata... Inabidi ukapimwe medula oblongata..
 
KOCHA KABET kikosi cha ovyo kabisa.mara 100 angeanzisha kile kilichoanza niger
 
Yaa, tumejitahidi. Tunampongeza mama kwa mtokeo mazuri. Kombe la dunia na mama. Mama anaupiga mwingi.
 
Serikali ya CCM iruhusu uraia pacha ili kuondokana na huu unyonge. Waachane na mitazamo yao ya kizamani kuhusu huo uraia pacha.
 
wewe goli la ziyech unasema uzembe wa kipa?upigajinhuo huwa anapiga aziz ki,na makipa wote uwajuawo,walifungwa,acha ujinga
 
Ilikuwa afungwe tano ama Saba, lkn kuchezea na team Ile iliyocheza nusu final za world cup na kufungwa Moja ninkujitahid, goal lingine tuliwasaidia

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
 
Ilikuwa afungwe tano ama Saba, lkn kuchezea na team Ile iliyocheza nusu final za world cup na kufungwa Moja ninkujitahid, goal lingine tuliwasaidia

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
Huna hoja. Bado unapuyanga. Kwakuwa brazil alipigwa 7 na Germany eti utegemee Wales atapigwa 10 na Germany eti kwakuwa tu ni mdogo kuliko Brazil??

Kujitahidi ni sare au ushindi, nje na hapo hakuna kitu. Kama umepigwa hakuna ulichofanya haijalishi ni chache au kibunda.

Mtu afeli mtihani umwambie kajitahidi kwakuwa kapata mbili badala ya sifuri kabisa?
 
Usajili ufanyiwe marekebisho;
1. Bashite
2. Mwigulu
3. Nape
Waongezwe kwenye kikosi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…