Kocha Taifa Star: Chonde Chonde Kazimoto, Taifa linakuhitaji

Kocha Taifa Star: Chonde Chonde Kazimoto, Taifa linakuhitaji

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Kauli hiyo ilitolewa jana na kocha msaidizi, Mtalamu Hemed Morocco, wakati akitangaza kikosi kitakachopambana na Malawi siku zijazo.
Namnukuu.. "Mwinyi Kazimoto umri wake bado ni mdogo kutangaza kuacha kulitumikia taifa na anachokifanya ni kujimaliza".. Pia alimsihi kurudi kulitumikia Taifa lake, kwani mchango wake bado unahitajika saaaana.
Nami naungana na Hemmed Morocco, kumsihi Mwinyi Kazimoto a.k.a Ball Dancer.. Ball Dancer taifa bado linakuhitaji sana.. Shime futa kauli yako.
 
Umri mdogo ni miaka mingapi,Kazimoto ameshazeeka kafanya uamuzi mzuri kuwapisha vijana

Kwani Mkuu, Mkwasa na Morocco hawawaoni hao viungo vijana.. Mpaka wampigie magoti Ball Dancer Kazimoto?
Naona Mkuu umeamua tu kubishana na Kocha bora kabisa kuwahi kushudiwa katika visiwa vya Zanzibar.. Na kumbuka hii ni kauli ya Benchi zima la ufundi la Taifa Stars linaloongozwa na Charles Boniphace Mkwasa.
Kila wakichekecha na mwenzake Mkwasa, wanaona kabisa kuna pengo la Pass Master, Kazimoto.
Shime tena Ball Dancer, kunjua moyo wako.
 
Yaan kwa mara ya kwanza nimekutana nae uyu kazimoto airport last year mmmh ule umri anasema anao ni wa kazi tu nadhan atakua ktk 37 yule apumzike tu akina dumayo mda wao sasa
 
Back
Top Bottom