Kocha Timu ya Taifa, Hemed Morocco awafukuza Mkoko, Lanso kambini kwa utovu wa nidhamu

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Kocha wa Timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, Hemed Suleiman 'Morocco' amewaondoa kambini nyota wake wawili kwa utovu wa nidhamu.
photo-output.jpeg

Katika taarifa iliyotolewa na ZFF, nyota waliofukuzwa ni Ibrahim Mkoko anayekipiga katika klabu ya Namungo FC na Abdallah Said (Lanso) wa KMC.

Utovu wao wa nidhamu uliotajwa katika taarifa hiyo ni kuchelewa kujiunga na kambi ya timu ya Taifa inayojiandaa na mashindano ya Mapinduzi Cup yanayotarajiwa kuanza rasmi Januati 3, 2025 msimu huu yakihusisha timu za Taifa, ikiwa tayari walisharuhusiwa na klabu zao.
IMG_2034.jpeg

Aidha, Morocco amemuongeza Ali Juma Maarifs (Mabata) anayekipiga kwenye kikosi cha Uhamiaji inayoshiriki Ligi kuu Zanzibar.

Heroes iliingia kambini Desemba 24 na jana ilianza rasmi maandalizi.
IMG_2030.jpeg
 
Kichwa cha habari:
Kocha wa timu ya taifa
Content: kocha wa timu ya taifa ya zanzibar
Ndugu mwandishi lengo lako hasa ni nini mbona unakuwa kama bloggers uchwara wa online tv
 
Kocha wa Timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, Hemed Suleiman 'Morocco' amewaondoa kambini nyota wake wawili kwa utovu wa nidhamu.
View attachment 3185664
Katika taarifa iliyotolewa na ZFF, nyota waliofukuzwa ni Ibrahim Mkoko anayekipiga katika klabu ya Namungo FC na Abdallah Said (Lanso) wa KMC.

Utovu wao wa nidhamu uliotajwa katika taarifa hiyo ni kuchelewa kujiunga na kambi ya timu ya Taifa inayojiandaa na mashindano ya Mapinduzi Cup yanayotarajiwa kuanza rasmi Januati 3, 2025 msimu huu yakihusisha timu za Taifa, ikiwa tayari walisharuhusiwa na klabu zao.
View attachment 3185665
Aidha, Morocco amemuongeza Ali Juma Maarifs (Mabata) anayekipiga kwenye kikosi cha Uhamiaji inayoshiriki Ligi kuu Zanzibar.

Heroes iliingia kambini Desemba 24 na jana ilianza rasmi maandalizi.
View attachment 3185660
Zanzibar sio Taifa since 1964
 
Seleman mwalim wameenda kumfungia huko team yake FOUNTAIN gate sasa hivi inafungwa hovyo hovyo

Tangu mwezi wa saba wanamuita ita
 
Back
Top Bottom