ibanezafrica
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,261
- 6,553
Vipi, amepata na kiatu cha dhahabu?Messi kapiga mawili kwenye fainali akiwa na miaka 35 ndio habari kubwa.
Kainua juu Kombe la Dunia,ndiyo habari ya mjini.Vipi, amepata na kiatu cha dhahabu?
Poleni sana maana naona mnatafuta kichaka cha kujifichia. Hukuona golden ball pamoja na kombe aliloinua?Vipi, amepata na kiatu cha dhahabu?
Kwenye final kinachoshindaniwa ni kombe,huoni kua hata baada ya mechi kuisha Mbappe hakua na furaha,kombe ndio muhimu kwenye final mkuu.Uzuri kila mwenye macho ameona. Hebu fikiria, kijana mdogo tu wa miaka 24 anapiga hat trik kwenye mchezo wa fainali mbele ya mchezaji mkongwe kama Lionel Messi!!
Uzuri kila mwenye macho ameona. Hebu fikiria, kijana mdogo tu wa miaka 24 anapiga hat trik kwenye mchezo wa fainali mbele ya mchezaji mkongwe kama Lionel Messi!!
Vipi, amepata na kiatu cha dhahabu?
No problem, Mbape amechukua kiatu cha dhahabu! Na Messi amefanikiwa kuchukua kombe la dunia akiwa na miaka 35; huku Mbape akifanya hivyo na miaka 18 tu.Nyie hamjui mpira, Mbappe tunamkubali sana lakini anahitaji jitihada beyond human limits, nidhamu, na muhimu kuliko yote kudra za Mungu kuweza kufika walau robo ya ambacho Messi na Ronaldo wameifanyia dunia ya mpira.
Mtu kama Messi kama ulibahatika kumuona wakati ana miaka 19, wakati anavaa jezi namba 30, baadae akavaa namba 19 long before hajaanza hata kuvaa namba 10, wakati anapiga hat trick mbele ya Madrid ilojaa wachezaji wakali wote ulokua unawajua, huwezi kumkweza Mbappe mapema hivi.
Mimi Messi nimeanza kumfuatilia game moja ya UEFA na Chelsea ilichezwa darajani, Chelsea ilikua na watu wana roho mbaya kuliko unavyoweza kudhania ila kijana miaka 19 alikua anaweza kutembea na mabeki hata wanne kwenye chaki na anafika anakokwenda fresh tuu, the rest ni historia.
Baada ya VAR kuwa introduced kwenye mpira na baada ya generation ya Messi na Ronaldo kupita, nitaacha rasmi kushabikia mpira, nitakua naangalia kama burudani halafu nitahamia tu UFC.