Kocha wa deiwaka malengo semi-final Cafcl

Simba lunyasi

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2022
Posts
385
Reaction score
840
Huu ndio ukweli wanasimba wenzangu mkubali au mkatae.. Tuna ombwe kubwa la uongozi pale Simba S.C
Tatizo la timu kukosa head coach paka sasa wakati ligi imeanza na tuna malengo yakufika mbali cafcl linatufanya tuonekane hatuko serious.

Karibu mwaka wa tatu huu uongozi umekuwa ukituhadaa kwa kutuletea makocha wa hovyo hovyo wa bei rahisi huku wakiwapa malengo makubwa na kwakujua kabisaa makocha hao hawataweza kuyafikia ili wapate sababu ya kuwafukuza na kisha kuja kuwadanganya wanachama eti kocha hajatimiza malengo ya klabu hivyo tumevunja mkataba nae

Kwa timu hii ya kina John Bocco, Jimmyson mwanuke, Gadiel Michael, Mzamiru, Erasto Nyoni, Mkude, Israel mwenda, Onyango,Ouatara na kocha ndio huyo deiwaka mgunda ndio tufike semi final cafcl[emoji848][emoji848][emoji848]??

Tuamke sasa, uongozi uliopo Sasa Simba S.C haufai mabadiliko yanaitajika haraka sana hasa pale juu kwa yule bi dada maana ameshapwaya pakubwa sana.

Mjumbe hauwawi..
Simba nguvu Moja[emoji123][emoji123]
 
Bora wewe umeongelea uongozi.
Kwa ujumla hatuna viongozi makini.Unaona tu jinsi wanavyonunua wachezaji. Unashangaa club kubwa kama Simba haina pesa ya kumsajili Manzoki ili wasaidiane na Moses Phiri inaenda kusajili mzungu kisha unasema apewe muda msimu mmoja!Huu si ni uhuni?Kama ni kutoa muda kwa wachezaji si msajili under 17 watanzania kisha ndio muwape muda.

Uongozi umefeli sana sihitaji hata kuwasikia.
 
Ko mgunda ni nani sasa kama sio head coach??mashabiki wa kizazi hiki mna shida sana
 
Mbn kwenye hao wachezaji hujataja sakho chama phiri okrah okwa au hawa sio wachezaji wa simba?
 
Kifika fina au nusu ya champions league inatakiwa kuwa project ya miaka mitatu. Hivyo basi tafuta bench la ufundi zuri, hapa sasa ubahili usiwepo maana kizuri gharama. Mambo ya kudanganyana kila leo tumepikea cv 100 ni uninga na i aonyesha watu hawajui mpira mafanikio yanapatikanaje. Unapaswa kujua who the best in ur industry is. Huwezi kila leo unafukuza kocha unaleta somjo za wame apply makocha mia hamna mzawa alie apply. Sifa za kijinga hizi.
 
Kuwa Juma mgunda ni kocha deiwaka pale Simba??
Halafu hizi habari za kufika caf champions league semi final huwa mnaota au mpo siriaz???
 
Ofcoz hoja hii inafikirisha Sana wa lunyasi wenzangu aise, Tena makocha wenyewe sasa Aina ya matola ushikaji na wachezaji umetamalaki, hiv makocha Hawa Akina nyoni au mkude wakizingua uwanjan wanaweza kuwakemea kweli kwa hii zero distance iliyopo baina ya wachezaji wazawa na makocha wetu, goja tuone tuendeko binafsi naona Giza Sana had Kuna wakat hata Hawa waangola naingiwa na kaubarid sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…