Kocha wa Ndanda aula Azam

Kocha wa Ndanda aula Azam

Casuist

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2014
Posts
1,189
Reaction score
2,970
ALIYEKUWA kocha wa Ndanda FC, Denis Kitambi ameula kwa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Azam, baada ya kupewa jukumu la kuiongoza timu hiyo.

Habari za uhakika kutoka Azam jana zilisema Kitambi ataanza kazi rasmi leo kwa kushirikaina na kocha Mganda George Nsimbe.

Kitambi alikuwa mwajiriwa wa Azam kama mchambuzi wa masuala ya soka. Azam iliachana na makocha wake Joseph Omog na Ibrahim Shikanda kwa madai ya kushindwa kufanya kazi yao ipasavyo.

Akizungumza na gazeti hili mmoja wa viongozi wa juu wa Azam, alisema uongozi umeamua kumpa Kitambi kazi hiyo.

"Bado tupo kwenye kutafuta kocha, lakini kwa sasa Kitambi atakuwa na timu akisaidians na Nsimbe," alisema kiongozi huyo.

Omog ndiye aliyeiongoza Azam kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Mei mwaka jana, lakini hakuweza kuipa mafanikio kwenye michuano ya kimataifa.

Mwaka jana ikishiriki michuano ya Kombe la Shirikisho iliishia raundi ya awali baada ya kufungwa na Ferroviario de Nampula.

Hilo lilijirudia mwaka huu ambapo ilitolewa mapema na El Merreikh ya Sudan kwa jumla ya mabao 3-2, ikishinda mabao 2-0 nyumbani kabla ya kufungwa mabao 3-0 Sudan.

CHANZO:
Habari Leo

 
Mmmh bora Omong

ule msemo usemao MCHAWI MPE MWANAO, umetimia, juzi kuna watu walianzisha thread humu ya kumsifia kuwa anaujua mpira, nikasema ule mpira wa kuchambua ukiwa ndani ya studio kila mtu anaweza ngoma ipo kwenye field. Ngoja tumpe muda,
 
ule msemo usemao MCHAWI MPE MWANAO, umetimia, juzi kuna watu walianzisha thread humu ya kumsifia kuwa anaujua mpira, nikasema ule mpira wa kuchambua ukiwa ndani ya studio kila mtu anaweza ngoma ipo kwenye field. Ngoja tumpe muda,

lets wait and see

hata hivyo kuwa kocha mzuri na kuwa mchambuzi mzuri sio lazima vifuatane
 
Back
Top Bottom