Kimsingi tunaweza kusema kwamba kocha ameshindwa kufikia matakwa ya mkataba.
Nilimsikiliza jana yeye mwenyewe, alisema kwamba mkataba aliokuwa ameingia na timu ya Polisi Morogoro ulikuwa unamtaka timu isifungwe mechi tatu mfululizo. Sasa bahati mbaya kabla ya mechi ya draw timu ilifungwa mechi tatu mfululizo.
Kwa kuzingatia matakwa ya mkataba ilibidi asimame kuifundisha timu.