Kocha wa simba awaka asema siwezi kumtumia Mo Ibrahim,hana nidhamu na simba sio timu ya sikukuu

Kocha wa simba awaka asema siwezi kumtumia Mo Ibrahim,hana nidhamu na simba sio timu ya sikukuu

Hata mimi nina wasiwasi kuna kitu hakiko sawa. Jamaa anaonekana ni mwenye nidhamu kabisaa.
Amekuwa akisema sijui mke wake anajifungua mtoto mara mwanaye kafa mara mtoto anaumwa

Uswahili huo na wazungu hawapendi excuses ndogo ndogo
 
Nadhani kuna ubaguzi huko simba wa kushughulikia matatizo.Kuna mchezaji alitolewa substitution akapitiliza jukwaani kwa hasira huku kila mtu anamshuhudia.Akafuatwa na viongozi waandamizi kubembelezwa akaweka earphone masikioni.

Sijasikia hatua yoyote ikic
hukuliwa na timu inayodai kuwa nidhamu ni kitu cha kwanza kwake.Hizo sheria inakuaje zinabaga watu?
 
Amekuwa akisema sijui mke wake anajifungua mtoto mara mwanaye kafa mara mtoto anaumwa

Uswahili huo na wazungu hawapendi excuses ndogo ndogo
Sio kweli! Mo amefiwa na mtto wake kbla ya kocha mzungu ajafika simba! Alifiwa na mwanae desemba kocha kaja januari
 
Huyu mzungu apunguze maneno "this is simba" atafukuzwa yeye na Mo abaki
 
Namfahau Mo ( nimecheza nae na pia tulisoma wote o'level) ni moja kati ya wachezaj wenye nidhamu ya hali ya juu... Somethng is wrong here!
Kwa nini asiwe muwazi? Kweli katika viongozi wote hana hata mmoja ambaye anaweza kumueleza kinachomsibu? Afunguke apate msaada hiyo inamuathiri hata yeye,
 
Nimemaliza nae form four mwaka 2010.
Mtafute basi umpe ushauri mzuri, sio vizuri kushindana na viongozi wa timu hata kama wao ndio wanamakosa.
Ni wajibu wa mchezaji kuhakikisha kocha wako na viongozi wengine wanakuthamini na kukuheshimu hata kama unataka kuihama timu.
Mo inampasa anyenyekee na kufanya juhudi mazoezini, kwanini wamtaje yeye tu wakati timu inawachezaji wengine pia.
Hata hao wengine wanakosea pia ila wanaomba msamaha kwa wakati na wanajirekebisha.
Kumbuka mchezaji ukishindana na viongozi wako wewe ndio unaumia, unashindwa kuisaidia timu, unashindwa kucheza, unashindwa kufurahisha mashabiki wako, unaua kiwango chako, hata kwenye bechi huonekani na mwisho wa mwaka timu inakuacha kukusajiri.
Mwambie ajirekebisha acheze mpira ndio kazi yake.
 
Back
Top Bottom