Kocha wa Simba SC anatakiwa kuingia na mbinu ipi kuhakikisha anapata ushindi dhidi ya RS Barkane?

Kocha wa Simba SC anatakiwa kuingia na mbinu ipi kuhakikisha anapata ushindi dhidi ya RS Barkane?

73' na 85' Ahly SC anapigwa msako wa hatari na Memolodi Sundowns FC, chupu chupu kupigwa goli la pili.
 
Morison aanze badala ya bwalya maana anapeleka mpira mbele, shabalala awe makini kushambulia maana jamaa wana winga zenye kasi wanaweza kupiga kaunta tukaumia .Mkude akianza atagharimu timu pia inonga anapaswa kuwa makini rafu iliyozaa goli hakupaswa kuicheza.
Timu inabidi icheze kwa spid sio mchezaji anakaa na mpira muda mrefu
 
Kweli waanze kwa ku press lakini wawe makini sana na counter attack za wale jamaa.

Wana mawinga wenye mbio, kina Tuisila Kisinda na wenzao kuwa nao makini, muhimu ni kutambua tu kama walitulizwa na Asec Mimosas goli tatu naamini hata Simba wakitulia wakatumia nafasi wanazopata watafanya jambo.
 
guvu moya kanji bai awaite wachezaji na kuwapa vitisho. ushindi utaibuka mkubwa tu
Huu ndo utani ambao tulikuwa nao toka zamani..!

Watani wa Jadi Simba na Yanga.

Lakini leo kuna washamba wamekuja kupenda mpira baada ya MO na GSM wana matatizo sana, kujenga hoja hawajui wala utani hawajui pia, zaidi ni Kutukana na Kejeli tu.

Kuna mmoja anajita Zero Zero kila nikimtadhimini..!
 
Simba itashinda [emoji881][emoji881][emoji881]

3- 0 uhakika hizi
 
Mashabiki wa Simba SC na Wadau wa soka, upi uchambuzi wako kuelekea kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya RS Berkane, utakaofanyika Jumapili ya March 13 kundi D kwenye dimba la Benjamin Mkapa.

Unadhani Kocha Pablo Franco Martin aingie na mpango, au mbinu ipi kuhakikisha anapata ushindi kwenye mchezo huu, ambapo Simba SC walipoteza kwenye mchezo wa kwanza ugenini kwa mabao mawili kwa bila.

Kwangu..Simba SC wanatakiwa kuanza kwa kupress kwenye mstari wa juu [High Press] hii itasaidia Back Line ya RS Berkane kutokuwa Comfortable na mpira hivyo pressing ya Simba SC itanza kufanikiwa kwa haraka zaidi kutokana Kasi ya Sakho kulia na Movement nyingi za Banda kushoto, kwasababu RS Berkane kuna uwezekano wa kupress mstari wa kati [Mid Block].

Na hapo inatakiwa kiungo wa chini awe na akili ya haraka kutoa msaada pembeni, na katika sehemu ambayo Simba SC inatakiwa kuwa makini na kufanyiwa kazi sana kwenye mazoezi ni mipira ya kutengwa (Set Pieces) mabao mawili kwa RS Berkane yalipatikana kwa njia hiyo.

Utabiri wangu Kikosini;

1.Manula.
2.Kapombe.
3.Hussein.
4.Onyango.
5.Inonga.
6.Mkude.
7.Sahko.
8.Mzamir.
9.Kagere.
10.Bwalya.
11.Banda.

Akiba;

Kakolaya, Israel, Nyoni, Wawa, Lwanga, Kanoute, Bocco, Kibu, Jimmyson, Morrison.

Yapi maoni yako kuhusu mtanange huu.

..Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana..[/b]
Maoni yangu kuhusu mtanange huu ni kwamba Pablo ujuzi ni ndogo kwa hilo uliloliona.
 
1. Manula
2. Kapombe
3. Zimbwe
4. Onyango
5. Inonga
6. Mkude
7.Sakho
8.Mzamiru
9.Kagere
10. Kibu
11. Efua Moriss

Sub: Kakolanya, Gadiel, Nyoni, Mwenda, Bocco, Jimson, Mhilu, Bwalya na Lwanga.

N:B
Timu icheze jihadi iache ujinga wa kupiga backpass 600 na square passes 500.

Tucheze mipira mingi ya kwenda mbele tena kwa kasi kubwa kama ya kipindi kile tunacheza na Kaizer Chiefs au As Vita club hapo Lupaso stadium.

Tucheze mpira wa kasi na kukaba wote huku tukianzia mashambulizi juu kuliko chini.

Pia Kocha ana kaujinga flani kanakofanana na kocha wa PSG kakuchelewa kufanya sub kwa mchezaji aliyeboronga au ambeye mpira umemkataa siku hiyo.

Aache kuwaanzisha Banda na Bwalya hawa hawana nguvu wala kasi inayotosheleza kupambana na Waarabu. Huwa wanachelewesha au kupoteza mipara kwa wepesi ukiwafanyia pressing.

Mwisho japo si kwa umhimu:

"Kamati ya roho mbaya iongeze mashambulizi ya mabomu nje na ndani kwa dakika zote 90 + kuliko yale ya Russia dhidi ya Ukraine."
 
Huu ndo mtazamo au uchambuzi tunataka, hivyo hatuna budi kuheshimu maoni kama haya.

Vile vile kuhusu kufanya mabadiliko ni kweli kuna kuchelewa fulani kitendo ambacho Kocha anatakiwa kubadilika.

Simba SC Nguvu Moja..!
 
  • Thanks
Reactions: K11
Tutumie zile zile mbinu zetu za kuspray hewa ya kuwalekeza mwili
Kama tulivyofanya kwako kwa miaka minne mfululizo ukakosa ubingwa..!

Kama ni hivyo si ukubali kuwa Simba SC Next Level
 
Kanoute anakitete miguuni asugue kwenye bench tu
Kocha ameanza naye kwenye game.
20220313_150334.jpg
 
Simba inapaswa kuingia na mbinu ya kushambulia (ili kupata magoli) na kuzuia (ili wasifungwe). Mnaonaje hii mbinu?
 
Ni sahihi ila ila huyu kocha anamahaba ya juu sana na kibu Kwaiyo kesho usitegemee kumuona banda hapo
Yes Utabiri wako umetimia Kibu anaanza Banda yupo benchi, wacha tuone..! Kila la heri Mnyama Mkali Mwituni.
 
Back
Top Bottom