Kocha wa Taifa Stars ametumia vigezo gani kumuacha Kampombe, Zimbwe, Mzize na Sure Boy na kuita kikosini wakalia benchi?

Kocha wa Taifa Stars ametumia vigezo gani kumuacha Kampombe, Zimbwe, Mzize na Sure Boy na kuita kikosini wakalia benchi?

Hata hao walioachwa wangeitwa, bado kusingetokea maajabu yoyote yale, maana Tanzania tumejaliwa wachezaji wa ndondo cup tu! Wachezaji wa viwango vya Kimataifa, hatuna.
Inabidi tusishiriki mashindano ya kimataifa Kwa Hali hii
 
Hao si wachezaji

Hata Manura kwa makosa yake hapaswi daka
 
Kocha ndiye atakayewajibika kwa lolote, kuanzia kuchagua kikosi, kupanga kikosi, matokeo mazuri na matokeo mabovu. Kama asipofikisha malengo, atawajibika kuachia nafasi au kufukuzwa
Kocha Hana hata mwez anawajibika Kwa lipi hapo lawama Kwa waliomchagulia majina tu
 
Yule dogo Kremensi sijui Kremlin wa Vyura fc anaweza, hakupaswa kumwacha. Hawa madingi wengine hakuna shida
 
Salaam,

Binafsi nimeshangazwa sana na uteuzi wa kikosi cha Taifa Stars, ambapo nimeona wachezaji ambao wapo kikosi cha kwanza kwenye timu zao (regular players) wameachwa haswa niliotaja hapo juu. Sio hivyo tu wachezaji hao timu zao zipo kwenye mashindano ya kimataifa wakiwalisha timu zao lakini kuna baadhi ya wachezaji hawana timu mpaka sasa mfano Feisal Salum, unamwitaje kwenye timu wakati hajacheza mechi za mashindano kwa muda mrefu?? tunaheshimu uwezo wa Feisal but anahitaji match fitness. Sure Boy aliwa perfect choice.

Baka na Kibwana kwenye timu zao sio wachezaji regular wanapambania namba Ili wawe wanaanza imekuwaje wanaonza kwe timu zao wameachwa na ila wanaotafuta namba wameitwa?? No way sioni sababu ya Kapombe na Mohamed Hussein kuachwa. (Sijazugumzia wachezaji wa timu za daraja la kati ambao Kwa Sasa hatukupaswa kuwafanyia majaribio hapa ni kufuzu)

Nimesikitishwa zaidi na kocha kumuacha kijana tunaetegemea aje kuwa hazina ya Taifa hili hapo baadae Clement Mzize kijana ambae anahitaji exposure kama hizi ili aanze kujenga confidence katika michuano ya kimataifa katika level ya timu ya Taifa. Unfortunately kocha wetu sijui ametumia kigezo gani kumuacha (Takwimu zake so far zinaongea vizuri). Japo Mzize huwa anatokea benchi ila mpira ni mchezo wa wazi kijana ana potential sana kwa ma-striker vijana wa kitanzania kwa sasa sijaona kama Clement Mzize.

Personally nimeshindwa kumuelewa kocha. aombe Mungu apate matokeo mazuri kwenye hizo mechi vinginevyo atalijua joto la mpira wa Bongo lilivyo.
Anahitaji kutu-prove wrong otherwise atapishana mlangoni na hao aiowaacha

Mungu ibariki Tanzania.
Ila kwa Kapombe, Sure Boy, Shabalala na Mzize Kocha katukosea sana Watanzania. Akifungwa atuombe radhi kwa kweli.
 
Kwa sasa Bongo hatuna forward kama Mzize.

Kwakweli ni huzuni kumuachia nje Ila sio mbaya always Taifa Stars inatakiwa kufungwa sio kushinda
 
Back
Top Bottom