Kocha wa Taifa Stars Amunike ameidhalilisha sana Simba SC katika Uteuzi wake hivyo siishangilii tena Taifa Stars hadi akiondoka / akifukuzwa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Huwezi ukaita Wachezaji Watatu ( 3 ) wa Simba SC halafu ukawaita Wachezaji Wanne ( 4 ) wa Yanga SC. Kuanzia leo namchukia rasmi huyu Kocha na naomba Mungu tufungwe mechi zote kuanzia sasa. Na huwa nikimchukia Mtu huwa namchukia kweli. Nilikuwa namvumilia sana huyu Kocha na Mbichwa wake mkubwa pamoja na Pua lake ila naona kwa alichokifanya leo ni ' dhihaka ' kubwa kwa Klabu yangu pendwa ya Simba SC.

Kwahiyo ndani ya Simba SC amewaona Wachezaji Watatu tu Kipa Aishi Manula, Kiungo Mdogo wangu Kipenzi Jonas Gerald Mkude a.k.a Xavi Hernandez wa Tanzania na John Raphael Boko tu pekee? Ina maana Mohammed Hussein Zimbwe Jr ' Tshabalala ' hakumuona? Ina maana Kiungo ' Fundi ' kabisa Hassan Dilunga hakumuona? Ina maana Beki mwenye Roho Mbaya Paul Bukaba hakumuona?

Kuanzia le siishangilii tena Taifa Stars na naomba ifungwe kila mechi itakazocheza hasa inayoanza hii na Uganda Cranes wiki chache tu zijazo. Kama Kocha huyu mwenye Chuki za wazi wazi na Simba SC na mwenye Mahaba mazito na Yanga SC akiondoka au akifukuzwa nitarejea Kuishangilia ila siyo kwa sasa. Kocha ' Mnafiki ' sana huyu na niwaambieni mapema tu TFF kwamba huyu Kocha Emanuel Amunike hatufai kabisa na mfukuzeni mapema kabla hatujamfukuza kwa ' Bakora ' pale Kwa Mchina ( Mama yangu Samahani ) pale Kwa Mkapa kama tulivyohimizwa tuuite.

Popote pale duniani Timu ya Taifa yoyote ile huwa inajazwa Kwanza na Wachezaji ama wa Timu iliyokuwa Bingwa katika Ligi husika ya hiyo nchi au inashiriki Michuano ya Kimataifa sasa huyu Bichwa Kubwa, Mimacho Kutumbua wenu na Pua Andazi Amunike ameita hao Wachezaji Wanne ( 4 ) wa Yanga SC kwa ' Vigezo ' gani? Yanga SC ndiyo Bingwa Mtetezi wa VPL ( sasa TPL ) hii inayoendelea? Yanga SC inashiriki Michuano ya Kimataifa kwa sasa?

Ameshaniharibia kabisa Siku yangu!

Nawasilisha.
 
Huwezi ukaita Wachezaji Watatu ( 3 ) wa Simba SC halafu ukawaita Wachezaji Wanne ( 4 ) wa Yanga SC. Kuanzia leo namchukia rasmi huyu Kocha na naomba Mungu tufungwe mechi zote kuanzia sasa.
mkuu, watakuwa wameitwa kwenye "taifa stars" za nje ya Tanzania.
 
Kiuhalisia kocha kaharibu Sana timu hasa Safari hii, Kweli wachezaji wa mbao wapo juu ya wale vijana wa Azam? Kweli hajib hafai? Kweli zimbwe Jr, Dilunga, Singano hawastahili? Lakini kocha huenda anasababu zake za msingi, tumpe muda

Daima toa bila kukumbuka na Pokea bila kusahau
 
Mwacheni kocha afanye kazi yake.
 
Genta acha ushabiki maandazi. Kikosi cha kwanza cha Simba kina Watanzania wangapi? Ukweli mchungu ni kuwa Simba ina wachezaji wa Kitanzania watatu tu; Manula, Mkude, na Boko, wengine wote huwa wanabadilishana kwa zamu- M. Hussein, Ndemla, Mzamilu, Kichuya nk.

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kina Dilunga anawaachaje?Hivi Erasto Nyoni unamwacha unampanga Adrew vicent , Gadiel hamna kitu angemwacha tu

Sent using Jamii Forums mobile app

Nitashangaa sana baada ya hii leo huyu Kocha ' Kutudhalilisha ' Sisi Wanasimba halafu bado Wana Simba SC sisi sisi tukawa tena tunaishangilia Taifa Stars. Tena nawaomba wana Simba SC wote hakuna kwenda Uwanjani kuanzia sasa na mechi ijayo Sisi sote tuishangilie Uganda Cranes ikiwa na Wachezaji wetu akina Okwi na Murshid. Kocha Amunike hatumtaki!
 
Write your reply...
mechi ishauzwa hiyo kama ile ya lesotho,tusubiri kudra za uganda la sivyo wapenzi wa mpira bongo tufanye shughuli nyingine...

kocha mnaijeria ha ha haaa we can't be serious aisee
Mbona Simba ilishawahi kuwa na kocha Mburundi. Au ndio nyani haoni kundule?!
 
Huyu Amunike atakua amehonga tff huyu ili apate hiyo nafasi. Haiwezekani ametoka kwao huko halafu aje ajifunzie ukocha kwetu. Tujiandae tu kisaikolojia siku hiyo kushindwa kufuzu wakati nafasi ipo wazi. Kiufupi huyu jamaa hana karama ya ukocha ingawa enzi zake aliwahi kucheza timu nyingi tu kubwa ikiwemo hiyo barcelona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…