Kocha wa Taifa Stars asema tumefungwa magoli machache sana

Kocha wa Taifa Stars asema tumefungwa magoli machache sana

mh.Mch. Msigwa: Uwendawazim n kufanya kitu kile kile kwa akil zile zile af utegemee mabadiliko

Mstaafu Mh.Al hajj Rais Mwinyi: tumekuwa kichwa cha mwendawazimu......Mzee wetu ALLAH amjaalie umri mrefu na afya, maneno yake yaana maana pana saana.wataalam wakiswahili tupeni elimu ya msemo huu na football letu
 
Kanuni ya mvuto. Unavutia vile unavyofanana navyo sio vile unavyovitamani. Uongozi mbovu huvutia watendaji wabovu. Akifukuzwa kocha tutegemee kumpata mwingine mbovu.
 
Tatizo ni malinzi...wala sio kocha...siku zote hua nasema....ni sababu ipi ilimfanya malinzi kumtimua Kim?

Mkuu kumlaumu Malinzi au TFF kwangu mie ninaona kama kuwaonea.. Tatizo ni kubwa mno na limewazidi nguvu sana.. Ni sawa na kumlazimisha Daktari kumtibu mgonjwa wa kipindupindu kwa kutumia vidonge vya aspirini..!

Sekta ya michezo imeathirika kama zilivyoathirika sekta nyingine hapa Tanzania (siasa, vyama vya jamii etc).. Mpira wa miguu tunaupigia kelele kwa vile tu ndo mchezo unaopendwa sana hapa na ndo maana kila mara tunaona mapungufu..! Na bahati mbaya sana tumekuwa wepesi wa kulaumu TFF na uongozi wake pale Taifa Stars inapofanya vibaya lakini tunakuwa wagumu kulaumu au kulalamika kwa sauti ya juu pale Simba, Yanga au Azam zinavyotolewa mapema kwenye mashindano ya kimataifa..

Huwezi kumlaumu Malinzi wakati serikali imeyaweka mbali mambo ya miichezo.. Hakuna sera wala mipango yeyote kutoka serikalini katika kukabiliana na shida hii kubwa ambayo inatuumiza kichwa watanzania.. Na hii inaletwa kwa sababu tu hatuna viongozi wenye vision na ubunifu wa juu nini kifanyike kubadiilisha hili tatizo.. Nilitegemea serikali iwahusishe wadau wote katika operation maalumu ya kutafuta kiini kilichosababisha tufike hapa na suluhisho la kutoka hapa tulipo.. Bahati mbaya michezo (na haswa mpira wa miguu) imegeuzwa kama ni sehemu ya watu kuvuna kwa maslahi yao binafsi..

Leo hakuna mdau yeyote mwenye jibu la moja kwa moja kwa sababu kuna sababu lukuki zilizotufikisha hapa.. Lakini ukweli utabaki pale pale, hata akija Michel Platini pale TFF hakuna ajabu ambalo ataweza kulifanya.. Inahitajika intervention ya serikali tena kwa kuipa kipaumbele operation hii kama ni kweli tunataka kutoka hapa tulipo..

Tutakapokuwa na serikali iliowekeza kwenye michezo na management yake then itakuwa rahisi kuwa na vilabu vyenye viongozi wanaojua kuendesha vilabu na ambao hawatakuwa na maslahi yao binafsi, tutakuwa na wachezaji wenye vipaji na wenye mapenzi ya dhati ya kucheza mpira, tutakuwa na TFF yenye viongozi wenye weledi wa kuongoza michezo na wenye vision na creative, marefarii wengi wenye beji za kimataifa na ambao watakuwa wanaitwa kuchezesha games sehemu mbali mbali za Afrika, viwanja vya mpira mikoani vyenye turf nzuri na zinaruhusu mpira kuchezwa comfortable na ligi za madaraja tofauti zenye ushindani mkubwa..
 
Mkuu sosoliso labda nikuulize kitu.

Unamfahamu Nehemiah Mchechu?

Anafanya kazi NHC,Shirika la serikali....Pamoja na kuoza kwa serikali katika maeneo mengi...Umeona uwezo wa Mchechu NHC?

Mkuu...huwezi kuiweka TFF pembeni katika failure ya Timu ya Taifa na Vilabu
 
Last edited by a moderator:
Mtabadili kila aina ya makocha, tatizo si makocha tatizo ni uongozi wa TFF.

Kiongozi wa TFF Jamal Malinzi ni mbovu na wanaomsaidia wote ni wabovu, hawana ubunifu na hawana muono wa kujuwa wapi pakurekebisha, wewe fikiri kiongozi wa mpira wa karne hii anatangaza kuwa tatizo ni jezi! Khaa!

Tanzania soka linaweza kukuwa kwa haraka sana, ni ubunifu na mipango ya haraka na ya muda mrefu inayotakiwa ifanyike.

Hawa viongozi wa soka wamefikia mwisho wa fikra zao, hawawezi, hawawezi, hawawezi.

cc Bishanga



Ni kweli uyasemayo ila nafikiri tatizo liko kwa wachezaji zaidi kwani mpaka leo hii wachezaji wetu bado wanadhani kuwa uchawi ni moja ya kipaji katika soka na ndiyo maana hawafundishiki/kukocheka. Watupwe tu baharini, tumewachoka.
 
Kwa hali hii tunapo elekea ni kupotea kabisa kwa soka la tanzania

TAKWIMU ZA HUYU KOCHA WA TIMU YA TAIFA


Kacheza MECHI =17

Kafungwa MECHI=8

Kashinda MECHI=3

Ame suruhu MECHI=6


Hapa inaonyesha ushindi wetu sisi ni suruhu. sasa najiuliza mwenyewe ni kweli MALINZI hayaoni haya matokeo mabovu ya timu yetu?
 
Mkuu Freeland, ninakubaliana na wewe Msechu amefanya mazuri akiwa kwenye mazingira magumu.. Lakini kwangu me ninadhani itakuwa sio sahihi kulinganisha shirika moja la na TFF.. Kuna mambo mengi ambayo yako nje ya uwezo na majukumu ya TFF ambayo serikali kwa kushirikiana na taasisi nyingine na wadau wangeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa sana..

Kunahitaji kuwe na programu ya michezo mashuleni ambapo huko ndo kunapoanzia kuwapata wachezaji wadogo ambao watawezwa kukuzwa kwa nidhamu ya michezo.. Hapa Serikali inapaswa kuwajibika kwa hili kwa kuweka mazingira mazuri ambayo ni kutengeneza mitala ya michezo, kutoa walimu wa michezo, kuhakikisha kuna viwanja vya kutosha kwa ajili ya vijana hawa na kuhakikisha wanapata muda wa kutosha kujihusisha na michezo.. Hapa TFF hawana uwezo wala ubavu wa kuyafanya haya..

Maana TFF hawawatengenezi wachezaji, wao kazi yao wanatakiwa kutengeneza mazingira mazuri katika management ya mpira wa miguu.. Hiyo ni pamoja na kuhakikisha kunakuwa na flow nzuri ya wachezaji kuanzia chini (under 17) ambao hawa sasa watakuwa wanapatikana toka mashule mbalimbali pamoja na football academies mbali mbali ambazo zitakuwa chini ya wadau tofauti..
 
Last edited by a moderator:
Twendelee kutazama Wenzetu..
Nadhani hiyo inatosha kwa muda uliopo..

Hata ukiondoa uongozi Mara mia moja, je wachezaji unao. Programu endelevu za michezo zipo na miundo mbinu ya kuwezesha haya ipoo..

Tusije kuwa tunalaumiana kila mwaka kwa masuala yale yale na kushangilia chenga tu na sio kushinda ktk mashindano muhimu..

Soka na michezo kwa ujumla katika nchi hii bado ni safari ndefu..

Uhondo wa haya tunayoyaota no kuingia na kushiriki...

Midomo tu hatutafika popote..
 
Kocha mmbovu,,uongozi pia mmbovu....embu fikiria kama Rais wa TFF anajisifia kwamba mafanikio kwamba mechi za Stars karibia zote zimeoneshwa kwenye luninga.....
 
Basi Jamal Malinzi aachie uongozi TFF kwa wanaoweza. Anawaumiza sana Watanzania.

cc Bishanga

ikiwezekana hata Rais wa tff aajiriwe nchi za nje kama ilivyo kwa kocha..ikiwa viongozi hawahawa wa siku zote, wataleta tena jezi zileee za kumfika ngasa magotini kipindi cha maximo..kwa sababu zilipanda kwenye viwango vya FIFA.
 
Back
Top Bottom