Kocha wa Yanga afungiwa kuiongoza timu yake katika mechi tatu. Mwamuzi aliyekataa goli la Ruvu Shooting afungiwa miezi mitatu

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Kamati ya Bodi ya Ligi Kuu ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi katika kikao chake cha Septemba 2, 2019 ilipitia matukio mbalimbali ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2019/2020 iliyoanza rasmi Agosti 24, 2019 na kufanya uamuzi ufuatao;

Mechi namba 9- Yanga 0 vs Ruvu Shooting 1. Mwamuzi Msaidizi Janeth Balama amefungiwa miezi mitatu kwa kushindwa kutafsiri sheria, hivyo kusababisha akatae bao halali lililofungwa na Ruvu Shooting katika mechi hiyo iliyofanyika Agosti 28, 2019 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Adhabu dhidi yake imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 39(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Waamuzi.

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ametozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kuvaa mavazi yasiyo nadhifu na ya heshima katika mechi hiyo, kinyume na Kanuni ya 14(2m) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu dhidi yake imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 41(13) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makocha.

Klabu ya Yanga imepewa Onyo Kali kwa kushindwa kuhakikisha Kocha wake Mwinyi Zahera anaongoza benchi la ufundi la timu yake akiwa katika mavazi nadhifu na ya heshima. Adhabu dhidi ya klabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Mkurugenzi wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ametozwa faini ya sh. 200,000 (laki mbili), kwa kuingia ndani ya uwanja (eneo la kuchezea) baada ya filimbi ya mwisho, kinyume na Kanuni ya 14(10) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu dhidi yake imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amefungiwa kuiongoza timu yake katika mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom kwa kutoa shutuma na kejeli kwa Bodi ya Ligi katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mechi dhidi ya Ruvu Shooting. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 41(9) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makocha.
**********

My take;
Alionywa sana, alishauriwa mno ila Kiburi chake, Dharau zake na Kujambishwa ( Kujazwa Upepo ) na Mashabiki wake wa Yanga SC kulimpa Jeuri zaidi na akadhani kuwa Yeye ni mkubwa kuliko TFF na kudhani kuwa labda TFF inamuogopa sana kama ambavyo Viongozi wake wa Yanga SC na Mashabiki wa Yanga SC wanavyomuogopa na Kumnyenyekea.

Habari za hivi punde tu kutoka Mtandao wa TFF na ule wa Shaffih Dauda zinasema kwamba Kocha wa Yanga SC Mwinyi Zahera amefungiwa Mechi ( Michezo ) Mitatu na pia Kupigwa Faini ya Shilingi Laki Tano ( Tsh 500,000/= ) huku pia akiwa amepewa ONYO KALI katika mambo mengine.

Nitawadharau mno wana Yanga SC kama watasema na wataona Kocha wao huyu ameonewa kwani kama ni Kuvumiliwa na TFF amefanyiwa sana ila sasa acheni anyooshwe. Ni Kocha aliyekosa Staha na Utu kwa Mamlaka ya Mpira nchini Tanzania na Bodi yake ya Ligi pia.

Na raha zaidi inakuja pale wakati leo TFF kupitia Kamati yake ya Maadili na Sheria zikila ' Kichwa ' cha Kocha Mwinyi Zahera na Kumpa Adhabu hiyo na Kutosimamia Timu yake katika Bench kwa Mechi 3, habari za Kuaminika kabisa kutoka katika Vyanzo vyangu hakika na muhimu ndani ya Yanga SC vinasema kuwa Uongozi wa Yanga SC nao umeshampa Kocha Mwinyi Zahera Mechi Tatu ambazo akifanya vibaya tu ( akifungwa ) wanamtimua haraka kwani tayari Kocha kutoka Serbia wanamalizana nae huku akiwa anasaidiwa na Kocha anayekuja kwa Kasi sasa nchini Kenya na ambaye alishawahi pia Kuichezea Yanga SC kwa Mafanikio makubwa Bernard Mwalala.

Natoa pongezi ( kongole ) kubwa wa TFF kwa Kumpa Kocha wa Yanga SC hii Adhabu na akome kabisa. Mbona Kocha wa Simba SC Patrick Aussems ambaye CV yake ni ya juu zaidi ya mara Saba ya CV ya Kocha Mwinyi Zahera Yeye hana matatizo ni Mstaarabu mno hadi nadiriki sasa Kupendekeza kwa TFF kuwa kama wataweza basi hata Jukumu la kuwa Kocha Mkuu wa Taifa Stars yetu wakiona inafaa wampe tu Yeye.

Safi sana TFF ya Rais Wallace Karia.
 
Mbona hujaelezea kafanya nini?
 
Hakuna Lolote
Yanga Ipo Kimya Haijasema Hayo Uliyoandika
 
Wabongo na kuwahi uzi sasa hapo umeandika nini iwapo hujasema katiwa hatiani kwa kosa gani? Ningekuwa mwanayanga ningekufuata huko tabata
 
Hiyo faini inaonekana haiko na kosa kubwa. Sisi hatuwezi sema kitu ambayo hutujui cause yake ni ipi.
 
ZAHERA AKUMBANA NA ADHABU

Kamati ya Bodi ya Ligi Kuu ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi katika kikao chake cha Septemba 2, 2019 ilipitia matukio mbalimbali ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2019/2020 iliyoanza rasmi Agosti 24, 2019 na kufanya uamuzi ufuatao;

Mechi namba 9- Yanga 0 vs Ruvu Shooting 1. Mwamuzi Msaidizi Janeth Balama amefungiwa miezi mitatu kwa kushindwa kutafsiri sheria, hivyo kusababisha akatae bao halali lililofungwa na Ruvu Shooting katika mechi hiyo iliyofanyika Agosti 28, 2019 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Adhabu dhidi yake imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 39(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Waamuzi.

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ametozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kuvaa mavazi yasiyo nadhifu na ya heshima katika mechi hiyo, kinyume na Kanuni ya 14(2m) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu dhidi yake imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 41(13) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makocha.

Klabu ya Yanga imepewa Onyo Kali kwa kushindwa kuhakikisha Kocha wake Mwinyi Zahera anaongoza benchi la ufundi la timu yake akiwa katika mavazi nadhifu na ya heshima. Adhabu dhidi ya klabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Mkurugenzi wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ametozwa faini ya sh. 200,000 (laki mbili), kwa kuingia ndani ya uwanja (eneo la kuchezea) baada ya filimbi ya mwisho, kinyume na Kanuni ya 14(10) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu dhidi yake imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amefungiwa kuiongoza timu yake katika mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom kwa kutoa shutuma na kejeli kwa Bodi ya Ligi katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mechi dhidi ya Ruvu Shooting. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 41(9) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makocha.

Chanzo : TFF
 
Ligi lenyewe la hovyo kama nini

Hii Ligi kuwa hovyo umejua baada ya Kocha Mwinyi Zahera ' Kusulubiwa ' hivi au hata kabla? Kuna Watu waliwahi Kusema kuwa Wendawazimu wengi nchini Tanzania ni Mashabiki wa Yanga SC hivyo kupitia huu ' Upuuzi ' wako uliouandika hapa nakubaliana na hao Watu.
 
Hao mbumbu wenzako?
 
Wanatengeneza mazingira ya ubwingwa kwa simba kama kawaida yao

Sijaona Timu ya Kuweza Kuizuia Simba SC isitetee tena Ubingwa wake kwa Msimu huu wa 2019 / 2020 hasa kwa aina ya Kikosi chake kilichosheheni Mafundi watupu. Labda kidogo Timu ambazo zitajitutumua Kutusumbua ila siyo Kutufunga ni Azam, Kagera, Mtibwa na KMC ila kuna Timu Moja ya Mafurikoni Ilala Dar es Salaam hiyo tutaifunga Goli 7 kwa 0 katika Mizunguko yote ya Ligi.
 
Makocha kuvaa suti kunasaidiaje kuinua soka letu?
 
Ligi la wachezaji 10 wa kigeni ratiba inapangwa kuangalia simba acheze lini
 
Huu ni mojawapo ya upuuzi niliowah kuushuhudia maishan mwangu
 
Kweli mkuu ni km vile walisema hakuna wa kuizuia simba Kwenye makundi ya klabu bingwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…