Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
KOCHA wa Yanga Mwinyi Zahera amesema anaweza kuachana na timu hiyo baada ya msimu huu kumalizika kutokana na wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kushindwa kumpa ushirikiano.
Zahera ambaye ni Kocha Msaidizi wa timu ya taifa ya DR Congo, alijiunga na Yanga mwishoni mwa msimu uliopita kuchukua mikoba ya aliyekuwepo George Lwandamina aliyetimka kwao Zambia. Kwa mujibu wa taarifa ya Zahera jana kwa vyombo vya habari, ameamua kuondoka akisema ni ngumu kuendelea kujitolea wakati wenye timu hawajitolei.
“Jisaidie na Mungu atakusaidia, sasa mimi naweza kuondoka kwasababu nimefanya mengi kuwasaidia, nadhani hakuna mtu atachukia kwa niliyofanya, nimewasaidia vitu vingi ila naona wao kama hawapendi kujisaidia,”alisema. Kocha huyo alifafanua kuwa hawezi kuendelea kama mashabiki na wanachama wanashindwa kuchangia timu kupitia mpango waliotangaza wa kuchangia kwa ajili ya kujenga kikosi cha msimu ujao.
Alisema walianza matangazo ya watu kuchangia na sasa ni karibu mwezi mmoja ambapo anashangazwa ni kiasi kidogo tu kilichochangwa cha Sh milioni 21, wakati yeye peke yake alichanga Sh milioni mbili na sio shabiki wala mwanachama. “Na sababu gani wamesema Yanga ina matajiri wengi? Wanasema Yanga ni timu ya wananchi, sasa wale matajiri wengi hawaoni kama kila mmoja akichanga kwa wiki moja tutakuwa na fedha nyingi sana na kufanya maajabu?,”alihoji.
Alisema zinahitajika dola milioni mbili za Marekani (Sawa na Sh bilioni 4.8) Mei kwa ajili ya kununua wachezaji wakubwa na kujenga uwanja wa mazoezi. Zahera alisema anasikitika baadhi ya wanachama na mashabiki wakilalamika kupata maumivu hasa pale timu inapofungwa lakini hawana mchango wowote.
UPDATES
Kocha Mwinyi Zahera amesema habari zinazozunguka kwenye mitandao ya kijamii ikiwepo Instagram, WhatsApp na Twitter kuwa anatarajia kujiunga na klabu ya Azam ni za uongo na za hovyo kwa maana hakuna suala kama hilo
Amesema hajawasiliana na Kiongozi yeyote wa klabu ya Azam, si kwa simu wala ana kwa ana na yeye hamfahamu Kiongozo yeyote wa Azam wala hakuna Kiongozi wa Azam nayemjua yeye zaidi ya kuonana tu uwanjani
Ameeleza kuwa si mara ya kwanza kwa habari kama hizi kusambaa, ni habari tu za uongo watu wanaandika labda kwa maslahi yao wenyewe lakini yeye bado ana mkataba na Klabu ya Yanga
Aidha, amewasisitizia Mashabiki wa Yanga wasiwe na wasiwasi na kuwa chochote kinaweza kufanyika muda wowote ila yeye mwenye atasema, ikiwa anaenda Congo au ana safiri basi ataeleza na kuweka mambo wazi