Kocha wa zamani wa Simba, Pablo Franco aipa siri ya Ushindi Simba dhidi ya Berkane 'cheza kwa akili na siyo nguvu'

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Kocha wa zamani wa Simba, Pablo Franco ambaye anaifundisha Al-Qadsiah ya Saudi Arabia, alisema Simba inatakiwa kucheza kwa akili na siyo nguvu pekee.

“Berkane ni timu yenye uzoefu mkubwa kwenye michuano ya CAF. Watachelewesha muda na watatumia mbinu nyingi kuvuruga kasi. Simba inapaswa kuwa na subira, lakini bado iwe na kasi kwenye uamuzi wa mwisho,” alisema Pablo aliyesisitiza Fadlu akiwa na mpango mkakati mpya wa kuibana Berkane na kutengeneza nafasi za mabao Simba itaishangaza Berkane na Afrika kwa ujumla.

Nyota wa zamani na kocha wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, alisema: “Huu ni wakati wa Simba kupambana kwa roho moja. Wachezaji wanapaswa kutambua kuwa historia haijengwi kwa maneno, bali vitendo.”

MSIKIE FADLU
Kocha wa Simba, Fadlu Davids alisema kikosi kimejifunza kutokana na makosa ya mechi ya kwanza na kipo tayari kwa marudiano.

“Tumefanya tathmini ya yale tuliyokosea, hasa namna tulivyoanza mchezo taratibu. Safari hii tunaanza kwa kasi, tunamaliza kwa kasi. Tunahitaji bao la mapema kuhamasisha mashabiki wetu na kuwavuruga wapinzani,” alisema.

Davids alisema atawapa uhuru baadhi ya wachezaji kubadilika ndani ya uwanja kutegemea na hali ya mchezo, jambo ambalo linaweza kuwa silaha ya kuishangaza Berkane.

MASTAA WALA KIAPO
Nahodha wa Simba, Mohammed Hussein, alisema: “Tuna deni kwa mashabiki. Tunaamini tunaweza kupindua matokeo haya. Hii ni fursa ya kuweka majina yetu kwenye vitabu vya historia ya klabu.”

Naye Shomary Kapombe aliongeza: “Tumewahi kucheza mechi ngumu zaidi ya hii. Tutaingia kwa utulivu na mpango mmoja kushinda na kutwaa kombe.”

Naye kiungo mchezeshaji Charles Jean Ahoua alisema: “Nimecheza mechi nyingi za ushindani Afrika Magharibi, lakini hakuna presha kama hii. Tuna dhamira ya kushinda na tutapigana hadi mwisho.”

1747984460750.png
 
Kocha wa berkane alishasema wachezaji wa 5imba wachovu hawawezi kupishana nao, tunasubiri sare ama kipigo kingine kwa Mnyama
 
View attachment 3342782
Tatizo akili wanazo?
 
Baada ya Mchezo kocha wa Simba aliongea vitu vya ajabu katika mpira.
Kitendo cha kusema Berkane wata juta kukosa Goli la tatu mojakwamoja amesha jitoa katika mashindano.

Inaonekana tathmini yake kwa Berkane ana wachukulia poa kama timu nyingine alizowahi kucheza nazo katika mashindano aya.
Berkane waliwazidi Simba katika maeneo mengi, Eneo kubwa na la hatari, Wanakimbia sana wakiwa na mpira na wakiwa hawana mpira na Wana wachezaji wengi skillful.

Fadru tayari ameshafungwa kabla ya kucheza mechi ya pili.
 
Back
Top Bottom