Ondoa haraka sana wachezaji hawa dirisha dogo.
1.Jimmyson Mwinuke
2.Gadiel Michael
3.Erasto Nyoni,
4.Jonas Mkude
5.Sadio Kanoute
6.Peter Banda
7.Victor Akpan
8.Nelson Okwa
9.Mohamed Quattara
10.John Bocco
11.Denis Kibu
Hawa ni wachezaji wa kawaida sana, wanachokitafuta viongozi watakipata, uchaguzi hauko mbali.
Sent from my SM-F916B using
JamiiForums mobile app
Kukata au kuondoa majina ya wachezaji sio kazi ngumu, kazi ni kupata replacement zao (nazungumzia wachezaji wa ndani).
Mimi naona kwenye ligi yetu kuna uhaba mkubwa wa wachezaji wazuri sana ambao ni watanzania.
Top performer wa Mbeya Kwanza alikua Kyombo, ameletwa (mashabiki wanasema hatoshi).
Top performer wa Kagera Sugar alikua Mhilu, wote tunajua kilichotokea.
Habari za Charles ilanfya, Adam Salamba na wengine bila shaka bado tunazikumbuka.
Inaweza kuwa hivyo kwa Lusajo, Sixtus Sabilo, George Mpole au kwa star mwingine yeyote yule wa mid table teams.
Kila wakati Kibu ananikera kwa uchezaji wake, swali la kwanza ambalo najiuliza, kama mchezaji wa aina hii anaitwa timu ya taifa, maana yake hao wengine kawazidi kwa namna moja au nyingine, je unamuachaje huyu ili usajili hao aliowazidi.... Nabaki kuvumilia tu.
Hebu tusaidie jambo moja....
Akitoka Mkude, unapendekeza aje kiungo gani wa ndani.....
Akitoka Kibu aje winga gani wa ndani ?
NB:
1. Naomba usinitajie wachezaji wa Azam na Yanga (maana kimsingi hizo timu haziwezi kumuuzia Simba mchezaji ambaye bado wanamtaka).
2. Sijamtaja Bocco na Nyoni kwa sababu wao kigezo ni umri, hawa hakuna namna ni lazima waondoke.