Kocha yupi kati ya hawa alikuvutia zaidi katika EPL?

Kocha yupi kati ya hawa alikuvutia zaidi katika EPL?

Pep amekuta Man city ina muda mchache chini ya miaka 2 toka ichukue ubingwa wa ligi(2014 chini ya Pellegrini City alikuwa bingwa).

Pia ameikuta timu iko top 4 ya Epl almost kwa misimu kadhaa mfululizo.

Njoo sasa kwa Morinho, huyu mwamba aliikuta Chelsea ni timu inayocheza isishuke daraja, pia timu ilikuwa na miaka 54 mara ya mwisho tangu ichukue ubingwa lakini msimu wake wa kwanza akamaliza nafasi ya 2 Epl, msimu uliofuata akawa bingwa wa Epl huku akiweka rekodi ya kufungwa goli 15 pekee na cleansheet 24.

Hakuishia hapo msimu uliofuata alibeba tena ndoo ya Epl mbele ya makocha vigogo Fergie, Rafa Benitez na Wenger.

Kwa mazingira hayo hiyo kazi anaiweza The special one pekee.

N.b

2002 Morinho alichukua Ueropa akiwa na kikosi cha kawaida cha Fc Porto

2003 Morinho alichukua Uefa akiwa na kikosi cha kawaida cha Fc Porto wakati Pep ameshindwa kupata ubingwa wowote wa Ulaya akiwa na timu bora ya Bayern Munich, pia amepambana muda mrefu kuchukua Uefa akiwa na City licha ya kuwa na kila kitu.

Morinho ndiye kocha PEKEE Ulaya ambaye amechukua vikombe vyote kwa ngazi ya klabu, kikombe cha mwisho amechukua mwaka jana akiwa na As Roma cha Uefa conference league.

Kwa hoja hizo HAKUNA kama Morinho.
Hao wengine iliwachukua muda mrefu kutoboa japo walikuwa na kila kitu.
Mourinho aliichukua Inter ikiwa ya kawaida kawaida japo ilikuwa moto, moto alokuja kuuweka pale ilikuwa ni hatari, kiasi kwamba wachezaji wanaonza first eleven hawana tofauti kubwa na wale waliopo benchi.

Sidhani kama itatoa Inter Milan bora kama ile, haikuwa na superstar yoyote yule ila jamaa akaendesha timu ikawa ya moto haswa.

Alikuja Spain, akabadili kabisa utawala wa Barca pale Spain.
 
Pep sio mwalimu,wapenzi wa soka plz tofautisheni mwalimu na Technician..Mchezaji gani alietoka kwenye mikono ya pep akaenda na moto uleule? Achana na messi aliemkuta akiwa na moto wake

Hawa kina f.torres,zincheko,Sterling,G.jesus,cancelo
Nafkiri pep amekuwa overrated sana.
 
Naichukia nyumbu,siipendi asheno...ila kiukweli HAWA makocha Fergie na Wenger walikuwa ni makocha haswaaa...hawa wengine ni wahuni TU,walitembelea na wanatembelea nyota za wamiliki za kuwa na pesa za usajili...

YNWA
Ofkoz Wenger na Sir Alex hawana mpinzani EPL kwa rekod za miaka iliyopita. Jamaa wamepika haswa na watu wakapikika.
 
Zama huja na kuondoka. Lakini legacy hubaki. Hapa kuna makocha wanne tofauti ambao kwa nyakati tofauti waliongoza vilabu vyao kutwaa mataji kadhaa ya EPL. Kila kocha alikuwa na rekodi zake pamoja na mbinu zake. Ni yupi unamkubali zaidi?

1. Sir Alex Ferguson - Man Utd
Huyu ametwaa mataji 13 ya EPL akiwa Man Utd. Aliifanya Man Utd itambe na kuogopwa sana EPL. Alitwaa mataji matatu mfululizo ya EPL mara mbili tofauti. Tangu kuondoka kwake Man Utd inalegalega.

2. Arsene Wenger - Arsenal
Wenyewe the gunners walipenda kumuita “Profesa” alileta mapinduzi makubwa ya namna ya uchezaji katika EPL. Nani asiyejua jinsi alivoitengeneza Arsenal na kuwa mwiba mkali Highbury usingeweza kutoka salama. Mpaka anasatafu alitwaa mataji mawili tu ya EPL

3. Jose Mourinho - Chelsea
Kipindi chake cha kwanza pale Chelsea mwaka 2004-2007 Jose alikuwa kocha mwenye rekodi lukuki.
Msimu wa 2005 aliweka rekodi ambayo mpaka leo haijavunjwa. Clean sheet 24 za EPL katika mechi 38 sio mchezo huku Chelsea ikiruhusu magoli 15 tu katika mechi 38. Chelsea ilikuwa haishikiki. Alitwaa mataji mawili mfululizo.

4. Pep Guardiola ( Man City )
Master Pep mpaka sasa ana mataji matano ya EPL. Kwasasa ndio ameishika EPL. Ameweka rekodi ya kufika point 100 kwa msimu katika EPL. Anacheza soka la kisasa mno. Huku akileta mbinu zake ambazo zamani hazikuwahi kuwa applicable na makocha wenzake.

Nani angeweza kuleta kipa ambaye anatakiwa kuwa na footwork nzuri kuliko kudaka, nani angeweza kumfanya full back aingie ndani kucheza kama kiungo, nani angeweza kuchukua taji la EPL bila ya kuwa na natural striker namba 9
Hayo yote Guardiola kayaweza kufanya na kafanikiwa.

Kocha yupi unamkubali zaidii?
View attachment 2701560
Pep Guardiola.
 
Pep amekuta Man city ina muda mchache chini ya miaka 2 toka ichukue ubingwa wa ligi(2014 chini ya Pellegrini City alikuwa bingwa).

Pia ameikuta timu iko top 4 ya Epl almost kwa misimu kadhaa mfululizo.

Njoo sasa kwa Morinho, huyu mwamba aliikuta Chelsea ni timu inayocheza isishuke daraja, pia timu ilikuwa na miaka 54 mara ya mwisho tangu ichukue ubingwa lakini msimu wake wa kwanza akamaliza nafasi ya 2 Epl, msimu uliofuata akawa bingwa wa Epl huku akiweka rekodi ya kufungwa goli 15 pekee na cleansheet 24.

Hakuishia hapo msimu uliofuata alibeba tena ndoo ya Epl mbele ya makocha vigogo Fergie, Rafa Benitez na Wenger.

Kwa mazingira hayo hiyo kazi anaiweza The special one pekee.

N.b

2002 Morinho alichukua Ueropa akiwa na kikosi cha kawaida cha Fc Porto

2003 Morinho alichukua Uefa akiwa na kikosi cha kawaida cha Fc Porto wakati Pep ameshindwa kupata ubingwa wowote wa Ulaya akiwa na timu bora ya Bayern Munich, pia amepambana muda mrefu kuchukua Uefa akiwa na City licha ya kuwa na kila kitu.

Morinho ndiye kocha PEKEE Ulaya ambaye amechukua vikombe vyote kwa ngazi ya klabu, kikombe cha mwisho amechukua mwaka jana akiwa na As Roma cha Uefa conference league.

Kwa hoja hizo HAKUNA kama Morinho.
Hao wengine iliwachukua muda mrefu kutoboa japo walikuwa na kila kitu.
Kuchukua muda mrefu kutimiza malengo na kuchukua mda mfupi kutimiza malengo ....unaona hio ni hoja kweli ...

Huyo morhno ni outdated manager ,Kwa Sasa hana uwezo wowote wa ku buttle na kina pep ...

Pep anajiamin na anabadilika kulingana na muda ,kiufupi pep hajakalili ni innovative by nature...anabadilika kulingana na mazingira..

Hao kina mo wamekalili mipira za kizamani mpaka sasa haajiliki na timu yeyote kubwa ,huyo mo Kwa mpira wa Sasa uliojaa makocha watata kama Carlo ,klopp hawezi chukua CL hata apewe madrid ..

Mo ni mtu wa kukalili mambo ,hataki kubadilika ,mbinu za mwaka 90 Bado anazitumia Karne hii ya modern football ,kiufupi kashapitwa na wakati ndio maana mpaka Sasa kashatimuliwa team kubwa spurs ,united ,...zote kashidwa kushine ...

Pep is above all fu**cking Coacher mentioned above ....pep is another level ....
 
Kuhusu Pep wengi watakupinga ila mambo yako hivyo ulivyosema.

1. Aliikuta Barca iloachwa na Frank Rjikard ikiwa na moto wa vijana wengi wazuri.

2. Alienda Bayern ikiwa bado ni mbabe wa Bundesliga na mpaka kesho bado watakuwa ni wababe wa bundesliga.

3. Kaenda Man City ikiwa bado ina tawala vizuri tu soka la EPL, hakutumia nguvu kubwa sana kuibadilisha Man City.

Yote ktk yote nakubali jamaa pia ni mwalimu mzuri, tena sana tu.
Kama pep hakutumia nguvu kuitransform city niambie ni kocha gani anaweza watumia kina akanji ,ake ,lapoter stone ,dias [emoji23] kuifungua real Madrid ,buyern munich ,kutawala soka ulaya na kuwin treble ....

ifike hatua muelewe pep ni master ,anatumia average player kuzinyoosha timu kubwa balani ulaya ...

Mfano akanji ,ake ,stone ..nje ya man city unahisi wanaweza kuonesha ule uwezo wanaoonesha ? ,,,System ya pep ndio imewafanya kuwa monster mzee ,angalia sterling alipo saizi ,sio yule sterling wa Chelsea [emoji23]...

Hakuna kocha yeyote anaweza kuifikisha man city pep alipoifikisha ,...

Kuna wajinga et Kwa kikosi cha man city kocha yeyote anaweza ,pumbavu Sana ,wewe unaweza watumia kina ake ,stone ,foden ,akanji ,kupiga team kubwa balani ulaya kama huna mbinu na system ya kimpira iliyonyooka ....maana Hao wote sio kwamba Wana individual brilliant kubwa no ,it's just pep system...

ifike hatua mjue pep = man city ,no any fuc**king cocher can train that average city player to be monster as they are ....,only pep transformed them ...
 
Naichukia nyumbu,siipendi asheno...ila kiukweli HAWA makocha Fergie na Wenger walikuwa ni makocha haswaaa...hawa wengine ni wahuni TU,walitembelea na wanatembelea nyota za wamiliki za kuwa na pesa za usajili...

YNWA
Wewe ni mpumbavu ,fuatilia kipindi hicho klub iliyokuwa na matumizi makubwa ya pesa ilikuwa ipi ....

Hio man UTD ikisema ichunguzwe kipind cha mwaka 1990 kwenye mafanikio yake ni vile hio FFP imeanzishwa 2008 ,walikuwa wahuni, wanamatumizi mkubwa ya pesa mno ,walikuwa wanatumia pesa vibaya mno ,walikuwa walitaka mchezaji Kwa namna yeyote wanampata Kwa gharama yeyote ,mishahara ilikuwa mikubwa wanalipwa ...

Kwa vile access ya kupata taarifa ilikuwa ngumu tofauti na Sasa kila kitu kipo wazi huwezi jua ....

Mambo ya kusema hakutumia pesa ni upumbavu kiwango cha juu [emoji23][emoji23][emoji23]hakuna club iliyofanikiwa bila kuwekaza pesa ...

Hata huyo klopp anajitamba sijui "I can't spend 80m for player" Leo anameza matapishi yake Kwa kununua kina Nunez ,vvd Kwa bei za kufuru [emoji23]....

Hakuna club sijui bahili , Liverpool,united ,Chelsea ,arsenal wote wanaspend money kama kawaida,Tena pesa nyingi tu ...ujinga wa kujificha et pesa ,sijui team flani inatumia pesa ni matumizi mabaya ya akili,taja team ambayo haitumii pesa na inafanya vzuri ...

Wewe ukipewa hata billion 20 unaweza tengeneza team shindani kama kichwani ni kilaza ? [emoji23]...

Money is not everything .....huyo morhno Kwa zile mbinu zake za kizamani ,na kuganda Kwa akili yake hataki kubadilika hata apewe billion 10 hawezi chukua CL kwa hii modern football yenye tactical Coacher Kama pep ,klopp , Carlo ....
 
Zama huja na kuondoka. Lakini legacy hubaki. Hapa kuna makocha wanne tofauti ambao kwa nyakati tofauti waliongoza vilabu vyao kutwaa mataji kadhaa ya EPL. Kila kocha alikuwa na rekodi zake pamoja na mbinu zake. Ni yupi unamkubali zaidi?

1. Sir Alex Ferguson - Man Utd
Huyu ametwaa mataji 13 ya EPL akiwa Man Utd. Aliifanya Man Utd itambe na kuogopwa sana EPL. Alitwaa mataji matatu mfululizo ya EPL mara mbili tofauti. Tangu kuondoka kwake Man Utd inalegalega.

2. Arsene Wenger - Arsenal
Wenyewe the gunners walipenda kumuita “Profesa” alileta mapinduzi makubwa ya namna ya uchezaji katika EPL. Nani asiyejua jinsi alivoitengeneza Arsenal na kuwa mwiba mkali Highbury usingeweza kutoka salama. Mpaka anasatafu alitwaa mataji mawili tu ya EPL

3. Jose Mourinho - Chelsea
Kipindi chake cha kwanza pale Chelsea mwaka 2004-2007 Jose alikuwa kocha mwenye rekodi lukuki.
Msimu wa 2005 aliweka rekodi ambayo mpaka leo haijavunjwa. Clean sheet 24 za EPL katika mechi 38 sio mchezo huku Chelsea ikiruhusu magoli 15 tu katika mechi 38. Chelsea ilikuwa haishikiki. Alitwaa mataji mawili mfululizo.

4. Pep Guardiola ( Man City )
Master Pep mpaka sasa ana mataji matano ya EPL. Kwasasa ndio ameishika EPL. Ameweka rekodi ya kufika point 100 kwa msimu katika EPL. Anacheza soka la kisasa mno. Huku akileta mbinu zake ambazo zamani hazikuwahi kuwa applicable na makocha wenzake.

Nani angeweza kuleta kipa ambaye anatakiwa kuwa na footwork nzuri kuliko kudaka, nani angeweza kumfanya full back aingie ndani kucheza kama kiungo, nani angeweza kuchukua taji la EPL bila ya kuwa na natural striker namba 9
Hayo yote Guardiola kayaweza kufanya na kafanikiwa.

Kocha yupi unamkubali zaidii?
View attachment 2701560
Julio
Pep Mnene.
 
Man city kabla ya pep ilikuwa na mataji mangapi na after pep ina mataji mangapi ?

Pep ameifanya EPL iwe farmers league.. kila msimu bingwa yeye tu
Akafundishe Watford ichukue makombe, baada ya Man City kununuliwa na Waarabu ndio timu imekuwa na jeuri ya pesa ya kununua kila mchezaji wanayemtaka. Hata akiondoka Pep, bado Man City ataendelea kubeba vikombe.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Spesho wani alikua balaa

Ilifikia kipind nilitaman apewe mgodi wa kiwira iwe mali yake kwa shart aifundishe stars

Mechi ya inter dhidi ya barca alidifens kuanzia dakika ya nne ilikua balaa

Mechi na Chelsea dhidi ya inter aliahid yey atakua kocha wa timu zote mbili mwishowe alionyesha umwamba kwa kuwadunda nje ndan
 
Back
Top Bottom