Kocha Zoran ampa onyo Kali John Bocco

Kocha Zoran ampa onyo Kali John Bocco

Acha Ramli chonganishi..chanzo cha taarifa yako?
Hakuna siri Duniani hapa mkuu, Simba Ni taasisi kubwa mno, so, mambo madogomadogo ya viwango vya wachezaji na kufungashiwa vilago lazima yafahamike hata kabla ya kuwekwa hewani, ndyo maana ya sources za media zilizoko huko Egypt
 
Mshambuliaji hatari Kibu Denis akiripoti kambini mapema, atasawazisha hayo makosa yote ya washambuliaji wenzake.
Bila Shaka huyu naye angekuwepo kule kambi washabiki wake wangeshililia moyo
 
Kocha Zoran ameendelea kugawa dozi kwa wachezaji, huku akimkomalia Bocco, akimtaka kuchagua moja kati ya kucheza mpira na kubakishwa kambini au awafuate kina Meddie Kagere, Chris Mugalu na Taddeo Lwanga waliofyekwa Misri.

Inadaiwa Bocco amekuwa akitegea sehemu ya mazoezi ya timu na inadaiwa imemfanya kocha huyo kukaa naye na kumtaka achague kucheza au kama anasumbuliwa na majeraha basi atafutiwe matibabu haraka kabla ya kufanya uamuzi wa kubaki naye Msimbazi au kufyekwa kama alivyofanywa kwa kina Mugalu waliorejeshwa nchini.

Katika hatua nyingine kocha huyo amesisitiza anataka atafutiwe washambuliaji wawili akiwamo namba tisa wa ukweli kutokana dili na Cesar Manzoki kuonekana kukwama na kusubiriwa kuongezwa katika dirisha dogo, jambo litakaloifanya timu isiwe na straika wa kutegemewa.

Awali, ilitarajiwa dili la Manzoki likamilishwe kwa Simba kutuma kigogo kwenda kuzungumza na uongozi wa Vipers ya Uganda inayommiliki mchezaji huyo, lakini mambo yamekwama kwa sababu klabu hiyo ya Uganda inataka ilipwe Dola 200,000 miezi miwili iliyobaki ya mkataba wake.
Hii taarifa ni uongo 100%
 
Back
Top Bottom