Kodi halali ni VAT nyingine zote ni wizi, amkeni

Kodi halali ni VAT nyingine zote ni wizi, amkeni

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Ukweli usemwe kodi ya uhalali katika nchi nyingi ni ile inayopewa jina la VAT na hutozwa pale unaponunua kitu.

Ila hapa Nyumbani Tz kuna mlolongo wa kodi zisizo na miguu wala kichwa ila zinameno na zinatumaliza wananchi.
Unaenda kununua mfano luku ya umeme mle ndani mna tozo tatu kuna hiyo ya kihalali VAT za wizi EWURA ,REA kuna na sasa kuna ya jengo.

Inawezekana wasomi wetu wamevamia mambo wasiyo na weledi nayo na ndio sasa wananchi wanapiga makelele au ni wizi wa makusudi ili kuteka hela za wananchi kwa nguvu,maana huu ndio kutawaliwa kwa nguvu.

Kodi au Ongezo la Thamani ni aina ya ushuru ambayo unatozwa na Serikali Kuu kwa wauzaji wa huduma na bidhaa kwa watumiaji. VAT hulipwa na watengenezaji watoa huduma na bidhaa, lakini mwishowe hupewa watumiaji ambao hununua huduma na bidhaa wakati wanalipia.

Ni Bora Serikali itoe mhemko wa kodi kwa vitu vyote,tuseme itamke kuwa kitu chochote kitakachohusu manunuzi kodi iwe ni 10%.

Ila kusema inabidi ulipie REA ili serikali ipeleke umeme vijijini,huo ni wizi , Hivi mlilazimishwa kugombea kuiongoza nchi hii ?
 
Utaambiwa tumevunja rekodi za makusanyo ... Ujinga mtupu ,
 
Sasa tuamkaje hebu tushauri Mkuu?.
Kuamka kupo kwa aina nyingi sana ,wahindi waligomea kununua bidhaa, huko ni kuamka na uhur wakaupata.

Hivyo namna ya kuamka sio kwa blah blah ,hivi unafikiri ukombozi unakuja kwakuhutubia kuhudhuriwa mikutano ,hayo ni makelele ya mlango ,hivyo kutafutwe makelele mengine.
 
Je Mnaweza kugomea kununua luku ?
 
Back
Top Bottom