Kodi kwenye Vocha na Miamala inaumiza Wananchi, ingeongezwa kwenye vinywaji


Siku zote anayeumizwa ni mwananchi wa chini linapokuja swala la bajeti
 

Bajeti Zanzibar hakuna kodi hata moja iliyoongezeka.

Huku kwetu shamba la bibi!

Mamburula yanayojifanya kila bajeti ikisomwa - "ni bajeti ya kumkomboa mwananchi," ni mzigo sana kwa nchi hii.

Kodi za sim cards, Bando hadi miamala? Ila wabunge na watawala kodi stahiki haziwahusu?

Wajameni, uhalali uko wapi?

Yapo mengi ambayo tungeweza kuyashinikiza vinginevyo na yakasimama.
 
Wewe ulitaka serikali itoe wapi pesa hasa ya kugharamia miradi ya barabara,afya na elimu?

Mimi nachoona kodi imekuwa kubwa ingepunguzwa kidogo afu waongeze kwenye bidhaa na huduma zinazosomeka kama luxury goods
 
Wewe ulitaka serikali itoe wapi pesa hasa ya kugharamia miradi ya barabara,afya na elimu?

Mimi nachoona kodi imekuwa kubwa ingepunguzwa kidogo afu waongeze kwenye bidhaa na huduma zinazosomeka kama luxury goods

"Kwamba serikali itoe wapi pesa za kugharimia ..."

Angalizo la msingi lilikuwa kodi Zenji hakuna moja imeongezwa huko serikali inatoa wapi pesa za kugharimia hayo?

Angalizo la pili kwetu wabunge na watawala hawalipi kodi stahiki kwa uhalali upi?

Serikali imeonyesha wapi kuwa kuna gharama zake zipi zisizokuwa za msingi itazipunguza?

Au yale yale ya kuzawadiana ma benzi ya 450m+ na majumba ya maBn/- + at our cost?

Miradi mikubwa iliyopo tusiyokuwa na uwezo nayo kihivyo ilipaswa kusimama au hata kutafutiwa mikono kama ina tija. Vinginevyo huyu ng'ombe mkamuliwa maziwa hata damu inayotoka itakata!
 
Mahitaji ya huduma tajwa hapo juu upande wa Zenji ni kidogo kuliko huku Bara
 
Hili ni tatizo kwa Waziri wa feza na raisi kwani hawezi kubuni mbinu za kuvutia mitaji kutoka nchi tajiri? na anafikiria kuongoza kodi kwenye sim, wale bibi kule vijijini wanaweka buku kwa mwezi unawaumiza, mtu mmoja anahudumia simu mpaka 10, kwani pesa anayopokea ndio anatuma kwa wazazi kijijini, anatoa kwa watoto 4 wako vyuo , kuna sim nyumbani, mke, nk, hii ni kumfilisi huyu mtu mmoja.

Punguza Kodi kwa waajiri ili waweze kuajiri vijana wengi na waongeze kodi, jamani hata hili hawawezi kufikiria?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…