Kodi na Tozo zinazowaumiza Watanzania: Tumekosea wapi ili tutubu?

Kodi na Tozo zinazowaumiza Watanzania: Tumekosea wapi ili tutubu?

Makadirio ilikua billion 120 kwa mwezi na mwezi huu wamekusanya bilioni 48. Maana yake Watanzania wengi wamegoma.
Watu wanakatwa pesa zao huku wanalia haijawahi kuwa BARAKA hata siku Moja.
Watu wamekosa plan B tu ila wangekimbia hizi Huduma.
 
Kibaya zaidi hawana ubunifu na njia ya kumkwamua mtu wa chini.

Ajira zimefutwa wala siyo issue sana kibaya zaidi hadi njia za kupokea pesa kutoka PAYPAL wamefunga.

Kuna fursa nyingi sana mtandao ila njia ya malipo ni PAYPAL. Unaacha pesa nje nje mpaka mwanaume unatoa machozi, unaomba hata ungezaliwa Kenya tu
Wanaacha kuwakaba wakampuni makubwa yanayomiliki Migodi ya Madini wanakuja kulia na Tabaka la kati simply hatuna sauti na ukipaza sauti unaishia kupakaziwa Uwongo mwingi
 
Kibaya zaidi hawana ubunifu na njia ya kumkwamua mtu wa chini.

Ajira zimefutwa wala siyo issue sana kibaya zaidi hadi njia za kupokea pesa kutoka PAYPAL wamefunga.

Kuna fursa nyingi sana mtandao ila njia ya malipo ni PAYPAL. Unaacha pesa nje nje mpaka mwanaume unatoa machozi, unaomba hata ungezaliwa Kenya tu
Hamia dini ya Budhist, kisha uombe uzaliwe upya ukiwa Kenya
 
The bottom line ipo kwenye matumizi ya anasa ya vigogo wa serikali, kuanzia magari ya kifahari yanayokunywa mafuta kama jini, safari na vikao visivyo na kichwa wala miguu inakuwa ni mwendo wa kulipana posho tu, kutumia mabilioni kugharamia bunge lisilo na tija ambalo kazi yake ni kugonga gonga meza kwa kila hoja inayotolewa na serikali, upigaji wa kufuru kwa watendaji waliokaa kwenye chaneli, kama ripoti za CAG zinavyoendelea kuibua uozo........kwa hiyo sahau kuhusu tozo kupungua maana hawa ni kama viwavi hawashibi.
 
Serikali iliyopatikana kwa njia haramu haiwezi kuwa na jema kwa wananchi. Wanajua hamkuwachagua, lazima mkomeshwe mshike adabu. Msije mkaleta tena choko za kudai haki ya kuchagua mnayemtaka.

Nchi inanyooshwa, wananchi mnanyooshwa, ili msiwasumbue watawala.
 
Ndugu zangu Watanzania tumekosea wapi mbona siku hadi siku mambo yanazidi kuwa tight sana mtaani huku. No pesa ukitumia ka hela kako kidogo unakutana na makato ya ajabu,ukiweka Vocha usalimie ndugu & jamaa napo tabu.

Day after day wanakuja na mbinu mpya sio kwa ajili ya kumpa ahueni Mtanzania bali wanazidi kutuongezea maumivu tu. Sitashangaa tena zikitoka takwimu za watu wasiokuwa na furaha Ulimwenguni Tanzania Tukaongoza no one is happy anymore kwa jinsi mambo yanavyoenda.

Viongozi wanaonekana kabisa hawapo kwa ajili ya wananchi bali wapo kwa ajili ya personal interests zao na sio ajabu kusikia kiongozi akijibu kwa ubabe kama hutaki nenda kaishi nchi nyingine tunaona kama kauli ndogo lakini inamaana zaidi ya 100 na zaidi. Kiongozi anayekwambia kaishi sijui wapi huko unadhani atakua na uchungu na wewe No.

Tumekua kama ng'ombe anayekamuliwa wamekamua maziwa yameisha sasa Chuchu zimeisha kutoa damu badala ya maziwa ila bado wanakamua tu.

Hakuwa mjinga mzee wetu Mkapa aliyefuta kodi ya Kichwa nakumbuka siku hiyo watu walishangilia sana na hata haikua hela nyingi almost mia 100-200 sasa assume kama mtu anayefurahia kufutwa kwa kodi ya Shs 100 leo unamkata mtu zaidi ya tsh 5000 kisa katumiwa hela.

SIKATAI KULIPA KODI NIKIWA KAMA MZALENDO ILA SIPENDI KULIPA KODI ZA DHULUMATI UKIONA KARIBIA ASILIMIA 89 YA WATU HAWA FURAHA DHIDI YA KODI/TOZO JUA HAPO UNAFANYA DHULUMA.

Tumkumbuke mtu mfupi Zakayo katika Biblia alikua mtoza/Mkusanya ushuru ila baada ya kuona hiyo kazi haina haki imejaa Dhuluma alichukua maamuzi ya kuachana nayo na kuambatana Na Bwana Yesu.

Rai yangu...Serikali rudini mezani mjadili tena tengenezeni Kodi/tozo ambazo kila Mzalendo atatoa huku akicheka/akifurahi.
Kazi iendelee tu....

NGOMBE ANAYA KAMULIWA .jpg
 
Harafu TRA hawathamini mchango wa walipa kodi huko kwingine Jan tunapata ujumbe wa kushukuru kwa kulipa kodi mwaka jana Tanzania January TRA wameanza na tangazo la kamata kamata Nchi nzima😂😂😂 unaona kabisa watu wa namna hiyo hawana mapenzi na si wazalendo na Nchi yao...wao ni kuanzisha figisu na Wananchi kila kukicha..
 
Back
Top Bottom