Ni kweli kabisa.
Na katika mfumo huo wa tax inatakiwa ku-incourage sana spending kwa kuwa uimara wa kiuchumi kwa taifa sio kiasi gani serikali inaingiza ila ni kiasi gani fedha inazunguka na katika mzunguko huo unaokota "chenchi" nyingi sana.
Hivi unajua kuwa ukimpa mtu elfu 10 halafu ukamtoza kodi ya shilingi elfu 3 kwa kila elfu 10 anayotumia, halafu huyo mtu akaiweka hiyo fedha chini ya godoro, uchumi unadorora??
Lakini ukimpa mtu shilingi elfu 10, halafu ukatoza kodi ya shilingi elfu 1 kwa kila mkono utakaoitumia hiyo shilingi elfu 10, na shilingi elfu 10 hiyo ikapita kwenye mikono kama ya watu 8 hivi, unakuwa umepata kodi ya shilingi elfu 8 kwa mizunguko ile ile, ongeza na ile elfu moja uliyotoza awali inakuwa jumla ni Tshs elfu 9??
Unafikiri kwa nini kiuchumi nchi kama Marekani inasisitiza sana watu wawe tabaka la kati kiuchumi??
Yaani haitaki kabisa kuwe na masikini wengi sana wala haitaki kabisa kuwepo na matajiri wakubwa wengi sana??
Ni kwa sababu watu wa tabaka la kati ni mahiri sana wa kutumia fedha zao kwa kufuja, hawajui kuwekeza, hawajui kubana matumizi, hawajui kama kuna kesho, wao maisha ni ufahari wa kujenga nyumba na kumikili simu nzuri na magari na simu za bei kali.
Hawawazi kujenga viwanda wala kumiliki makampuni.
Sasa ukitaka kuwaweza hawa, we wapunguzie kodi halafu wamwagie hela za kutosha, uone jinsi fedha itakavyozunguka mtaani.
Utaokota kodi japo ndogo ndogo ila itakuwa mara 5 ya ile uliyoitegemea awali.
Kibongo bongo sijui wataalamu wetu wa kiuchumi wanafeli wapi.