Kodi ya Fremu alipe directly mmiliki wa Frem na sio mpangaji

Kodi ya Fremu alipe directly mmiliki wa Frem na sio mpangaji

Ushauri wangu kwa Waziri wa fedha @Dr Mwigulu Nchemba na @tratanzania wafikirie namna ya kufanya hii With holding tax iwe inakusanywa na Manispaa au Serikali za mitaa kwa sababu ni imekuwa ni mzigo na dhuruma kwa Wafanya biashara na Wajasiriamali wanaobebeshwa huu mzigo wa kulipa With holding tax. Kwa sababu Barua ya utambulisho kwenda serikali za mitaa mfanyabiashara anaichukua kutoka TRA na anapoenda kuijaza Serikali za mitaa ni lazima aende na mkataba wa pango. Sasa pale ndipo unapotakiwa uwekwe utaratibu mzuri wa kuichukua hiyo pesa kutoka kwa Mmiliki wa fremu. Au Uandikishwaji wa Mkataba wa pango ufanyike Serikali za mitaa na pale Serikali za mtaa wachukue kodi ya withholding kutoka kwa Mmiliki.
 
Atakusumbua huyo mweupe kichwani,hao ndio wapangaji ambao wakinunua umeme pia wanataka ile kodi ya jengo buku jero alipe mwenye nyumba, nna mpangaji wangu mmoja anajifanya mchumi kutwa kuniuliza nitamfidia vipi kodi ya jengo ya kila mwezi, nimemuambia ngojea mkataba ukaribie mwisho tutajua
We mzee. Nimecheka sana 🤣 🤣 🤣
 
Ngoja waje wajuzi
Ukitaka kukata leseni ya biashara ni sharti uende na mkataba wa pango hata kama fremu ni yako lazima uwe na mkataba wa pango ili process zingine zifuate zikiwemo za kufanyiwa makadirio

Ndio maana nikasema mbuzi kafia kwa mchoma mishkaki maana utakuwa huonelewi ila unalipa kwa haki bin haki
 
Asante 🙏
 
Back
Top Bottom