Kodi ya Jengo au Kodi ya Mita ya LUKU?

Kodi ya Jengo au Kodi ya Mita ya LUKU?

yello masai

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2016
Posts
3,662
Reaction score
3,715
Binafsi sina jengo, ila kuna sehemu nimeweka umeme kwa ajili ya kazi zangu. Lakini sio kwenye jengo maana kazi hii nafanya sehemu ya wazi.

Sasa bwana leo nikasema ngoja ninunue umeme wa 2,200 nione kama nitakatwa kodi ya jengo wakati sina jengo.

Sijaamini kilichotokea, umeme wa 2,200 nimepata unit 0.6 kama inavyoonekana hapa chini.

Ushauri: Naishauri serikali kwa kuwa inahitaji hii kodi, isiite kodi ya jengo, iiteni kodi ya Mita ya LUKU. Kuna wengine tuna mita ila hatuna majengo.

TANESCO

IMG_20210821_082207.jpg
 
Hahahaa duh! Yani Tsh 200 ndo imenunua umeme! Tuna haki yakumkumbuka JPM na soon Service Charge itarudishwa kwa mwennendo huu ata bwawa la Nyerere pale rufiji likiisha halitakuwa na msaada wowote zaidi bei ya uneme itapanda.
 
Yaani ni balaa
 
Kuna udhaifu mkubwa sana kwenye hii kodi .. In fact sio kodi ya jengo ni kodi ya meter ni ile service charge imerudi kwa mlango mwingine
Imagine nyumba yenye vyumba vitano na kila chumba kikawa na luku yake maana yake hapo sio 2000 bali ni elfu 10 kwakuwa kila meter itachajiwa
 
Binafsi sina jengo, ila kuna sehemu nimeweka umeme kwa ajili ya kazi zangu. Lakini sio kwenye jengo maana kazi hii nafanya sehemu ya wazi.

Sasa bwana leo nikasema ngoja ninunue umeme wa 2,200 nione kama nitakatwa kodi ya jengo wakati sina jengo.

Sijaamini kilichotokea, umeme wa 2,200 nimepata unit 0.6 kama inavyoonekana hapa chini.

Ushauri: Naishauri serikali kwa kuwa inahitaji hii kodi, isiite kodi ya jengo, iiteni kodi ya Mita ya LUKU. Kuna wengine tuna mita ila hatuna majengo.

TANESCO

View attachment 1900968
Inaumiza Sana, ila tutafika TU, Hamna namna!
 
Kuna udhaifu mkubwa sana kwenye hii kodi .. In fact sio kodi ya jengo ni kodi ya meter ni ile service charge imerudi kwa mlango mwingine
Imagine nyumba yenye vyumba vitano na kila chumba kikawa na luku yake maana yake hapo sio 2000 bali ni elfu 10 kwakuwa kila meter itachajiwa
kwa mtazamo wangu ilitakiwa system imruhusu mtumiaji aingize namba ya nyumba kwa sababu nyumba moja haiwezi kusajiliwa zaidi ya mara moja.
 
Ndiyo. Ibadilishwe jina, iitwe kodi ya meter.
 
kwa mtazamo wangu ilitakiwa system imruhusu mtumiaji aingize namba ya nyumba kwa sababu nyumba moja haiwezi kusajiliwa zaidi ya mara moja.
Point kubwa sana hii ambayo mamlaka haikuizingatia
 
Vinginevyo waseme ni kodi ya ardhi au eneo lililowekewa LUKU.......wanaacha kuchukua kodi kwenye makampuni makubwa na yale yanayovuna madini wanaleta utitiri wa tozo kwa wananchi wa kawaida.
 
kwa mtazamo wangu ilitakiwa system imruhusu mtumiaji aingize namba ya nyumba kwa sababu nyumba moja haiwezi kusajiliwa zaidi ya mara moja.
Kweli mfano mimi nakaa kwenye appartment tupo familia nane( 8)
Wote tuna luku zetu kila mmoja
Akinunua luku anakatwa
So painfull jamani[emoji24][emoji24][emoji24]
 
Back
Top Bottom