Kodi ya majengo kupitia luku iliyoletwa kinyemela, imeondolewa kinyemela!!

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, Shalom!!

Lile ongezeko la TSH 500 lililoletwa kinyemela miezi miwili iliyopita, imeondolewa kinyemela kimya kimya bila taarifa yoyote.

Ikumbukwe kuwa, ongezeko hili halikuletwa kupitia Utaratibu wowote kisheria, baada ya kelele na malalamiko mengi Toka Kwa wananchi, imeondolewa bila ufafanuzi wowote.

Hapa ndipo tulipofikia kama nchi, kundi au viongozi kadhaa kwenye Taasisi au wizara za Serikali kumbe wanaweza kuongeza Kodi yoyote watakavyo na wasihojiwe na yoyote bila hatua yoyote kuchukuliwa dhidi Yao.

Tunahitaji majibu sahihi.

Karibuni 🙏
 
Na hii imekaajeee? Unit 28 mpaka unit 22
1000336608.jpg
 
Na hii imekaajeee? Unit 28 mpaka unit 22
View attachment 3062571

Pia kukimbia Kwa units tulikoambiwa watoto wametoka shule nako kukoje?

Walichochukua kinyemela wakirudishe, fidia juu na wawajibishwe.

Wako kama wanatuona manyani tu.

Viva Bangladesh ambako yule sheikh mmama katili yule, hatimaye katambua nchi ni ya wananchi!
 
Wabongo wazito kuelewa,Tanesco walishatolea maelekezo.Kipindi mfumo wa kodi za majengo unaingizwa kwenye manunuzi ya umeme,baadhi ya mita nyingi zilichelewa kuunganishwa toka mwaka mpya wa serikali,hivyo madeni yote kulipwa mwaka mpya wa serikali,Na si unavyodai kuwa imeondolewa kinyemela,.
 
Kwa hiyo kama nmewekewa umeme mwezi wa kumi nalipa kuanzia mwezi wa saba nane na tisa?
 
Mbona walitoa ufafanuzi, hakukuwa na ongezeko. Lilikuwa ni deni la mwezi Julai mwaka jana kwakua sheria ilichelewa kuanza kutekelezwa.
 
Kuna kubadilishiwa mita na kupoteza unit zako zilizobaki. Ahadi yao ni kurudishiwa unit kwa kutumiwa sms jambo ambalo halifanyiki.
 
Wabongo wazito kuelewa,Tanesco walishatolea maelekezo.Kipindi mfumo wa kodi za majengo unaingizwa kwenye manunuzi ya umeme,baadhi ya mita nyingi zilichelewa kuunganishwa toka mwaka mpya wa serikali,hivyo madeni yote kulipwa mwaka mpya wa serikali,Na si unavyodai kuwa imeondolewa kinyemela,.
Mimi nimevuta umeme na miez kama sita iv na mimi Nipo kwenye hilo den ama?
 
Salaam, Shalom!!

Lile ongezeko la TSH 500 lililoletwa kinyemela miezi miwili iliyopita, imeondolewa kinyemela kimya kimya bila taarifa yoyote.

Ikumbukwe kuwa, ongezeko hili halikuletwa kupitia Utaratibu wowote kisheria, baada ya kelele na malalamiko mengi Toka Kwa wananchi, imeondolewa bila ufafanuzi wowote.

Hapa ndipo tulipofikia kama nchi, kundi au viongozi kadhaa kwenye Taasisi au wizara za Serikali kumbe wanaweza kuongeza Kodi yoyote watakavyo na wasihojiwe na yoyote bila hatua yoyote kuchukuliwa dhidi Yao.

Tunahitaji majibu sahihi.

Karibuni 🙏
Mbona mimi mwezi huu nimekatwa sh 2000?
 
Wabongo wazito kuelewa,Tanesco walishatolea maelekezo.Kipindi mfumo wa kodi za majengo unaingizwa kwenye manunuzi ya umeme,baadhi ya mita nyingi zilichelewa kuunganishwa toka mwaka mpya wa serikali,hivyo madeni yote kulipwa mwaka mpya wa serikali,Na si unavyodai kuwa imeondolewa kinyemela,.
Niko hapa napitia comments za mazombie mpaka nashangaa. Eti lililetwa kinyemela na kuondolewa kinyemela! Watanzania tuna mtindio wa ubongo! Hiki kitu kilielezwa kabisa na wakasema ni mwezi mmoja tu! Kizazi hiki cha malalamiko sijui kitaisha lini?
 
Back
Top Bottom