Kodi ya majengo kupitia luku iliyoletwa kinyemela, imeondolewa kinyemela!!

Kodi ya majengo kupitia luku iliyoletwa kinyemela, imeondolewa kinyemela!!

Salaam, Shalom!!

Lile ongezeko la TSH 500 lililoletwa kinyemela miezi miwili iliyopita, imeondolewa kinyemela kimya kimya bila taarifa yoyote.

Ikumbukwe kuwa, ongezeko hili halikuletwa kupitia Utaratibu wowote kisheria, baada ya kelele na malalamiko mengi Toka Kwa wananchi, imeondolewa bila ufafanuzi wowote.

Hapa ndipo tulipofikia kama nchi, kundi au viongozi kadhaa kwenye Taasisi au wizara za Serikali kumbe wanaweza kuongeza Kodi yoyote watakavyo na wasihojiwe na yoyote bila hatua yoyote kuchukuliwa dhidi Yao.

Tunahitaji majibu sahihi.

Karibuni 🙏
Kwa msiofuatilia taarifa mbalimbali ndio mtasema limeondolewa kinyemela, lakini ungejishughulisha kutafuta habari ungeijua kuwa TANESCO waliishalitolea ufafanuzi zamaaaani!!!
 
Back
Top Bottom