Mimi nina Kajumba kangu huku uswahilini, kwa sababu ya ufinyu wa eneo nilijiongeza nikawekwa kaghorofa. Sasa serikali inanitaka nilipe elfu 15 kila mwezi. Yupo jirani yangu aliwanunua watu na kupata eneo kubwa, kuliwekea Uzio na kushusha mjengo wa kisasa wa nguvu.
Thamani ya jengo la jirani inaweza kuwa mara tano ya kaghorofa kangu, yeye atakuwa analipa buku jero kwa mwezi!
Sasa nawauliza hawa wataalam wetu wa kodi wametumia kigezo gani cha kutuadhibu wenye ghorofa? Kujenga ghorofa ni ishara ya utajiri na nyumba ya chini ni umaskini?
Nina mashaka na mfumo wa elimu wetu, huenda unazalisha wajinga zaidi