Kodi ya majengo ya ghorofa ni dhulma, haikubaliki

Kodi hii (Property Tax) anayehusika kulipa ni mmilikaji wa jengo na wala si mpangaji. Sasa iweje serikali imtoze mpangaji kupitia malipo ya LUKU? Sheria inaruhusu? Kwanini isimkabe huyo mwenye mali?
 
Kwa ujumla wake tu kodi ya majengo ni wizi. Maana umenunua ardhi kwa hela yako, umenunua vifaa vya ujenzi kwa hela yako (na hivyo vifaa tayari vimeshatozwa kodi za kila aina), unajenga nyumba kwa hela yako!
Sasa kwa nini ulipe tena kodi ya majengo kila mwezi!! Huu ni wizi.

Kama serikali inapenda kutoza kodi za majengo, ijenge nyumba zake nchi nzima na kuwapangisha watu wenye uhitaji. Ila siyo kuibiana mchana kweupe kupitia hizi sheria zao za kipuuzi.

Yaani ni wizi wizi ,kuna kodi ya Ardhi na Kodi ya Majengo.

Kodi ya Ardhi mwisho kulipa June 30(Viwanja vya kupimwa) kila mwaka ,kodi ya Majengo wanakata kwenye Umeme.....Najiuliza tu kwanini ulipe kodi ya Jengo na Ardhi kwa Pamoja,kwani Nyumba inaelea hewani? Kama bado haujajenga means utalipia kodi ya Ardhi(kwa viwanja vilivyopimwa) sasa ukija kujenga means utalipia kodi ya jengo ambayo itareplace kodi ya ardhi maana nyumba haujengi hewani.
 
Kwa ujumla wake tu kodi ya majengo ni wizi. Maana umenunua ardhi kwa hela yako, umenunua vifaa vya ujenzi kwa hela yako (na hivyo vifaa tayari vimeshatozwa kodi za kila aina), unajenga nyumba kwa hela yako!
Sasa kwa nini ulipe tena kodi ya majengo kila mwezi!! Huu ni wizi.

Kama serikali inapenda kutoza kodi za majengo, ijenge nyumba zake nchi nzima na kuwapangisha watu wenye uhitaji. Ila siyo kuibiana mchana kweupe kupitia hizi sheria zao za kipuuzi.
Haya machungu unayo pitia ni majibu ya wabunge walio ingia bungeni kwa wizi wa kura. Badala ya bunge kuisimamia serikali wamekuwa watetezi wa chama cha mapinduzi na serikali yake
 
Mimi nina Kajumba kangu huku uswahilini, kwa sababu ya ufinyu wa eneo nilijiongeza nikawekwa kaghorofa. Sasa serikali inanitaka nilipe elfu 15 kila mwezi. Yupo jirani yangu aliwanunua watu na kupata eneo kubwa, kuliwekea Uzio na kushusha mjengo wa kisasa wa nguvu.

Thamani ya jengo la jirani inaweza kuwa mara tano ya kaghorofa kangu, yeye atakuwa analipa buku jero kwa mwezi!

Sasa nawauliza hawa wataalam wetu wa kodi wametumia kigezo gani cha kutuadhibu wenye ghorofa? Kujenga ghorofa ni ishara ya utajiri na nyumba ya chini ni umaskini?

Nina mashaka na mfumo wa elimu wetu, huenda unazalisha wajinga zaidi
Hii nchi kila mtu analialia sasa kodi alipe nani , we umetaka ghorofa taratibu ndio hizo zifuate
 
Kodi hii (Property Tax) anayehusika kulipa ni mmilikaji wa jengo na wala si mpangaji. Sasa iweje serikali imtoze mpangaji kupitia malipo ya LUKU? Sheria inaruhusu? Kwanini isimkabe huyo mwenye mali?

Mtakabana wenyewe [emoji3][emoji3][emoji3].

Hawa ndo aliowasema Ndugai wenye makalai wanaenda kufanya negotiations na kutultea hizi kodi. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa ujumla wake tu kodi ya majengo ni wizi. Maana umenunua ardhi kwa hela yako, umenunua vifaa vya ujenzi kwa hela yako (na hivyo vifaa tayari vimeshatozwa kodi za kila aina), unajenga nyumba kwa hela yako!
Sasa kwa nini ulipe tena kodi ya majengo kila mwezi!! Huu ni wizi.

Kama serikali inapenda kutoza kodi za majengo, ijenge nyumba zake nchi nzima na kuwapangisha watu wenye uhitaji. Ila siyo kuibiana mchana kweupe kupitia hizi sheria zao za kipuuzi.
Jamaa ana kitu huyu asipuuzwe
 
Mimi nina Kajumba kangu huku uswahilini, kwa sababu ya ufinyu wa eneo nilijiongeza nikawekwa kaghorofa. Sasa serikali inanitaka nilipe elfu 15 kila mwezi. Yupo jirani yangu aliwanunua watu na kupata eneo kubwa, kuliwekea Uzio na kushusha mjengo wa kisasa wa nguvu.

Thamani ya jengo la jirani inaweza kuwa mara tano ya kaghorofa kangu, yeye atakuwa analipa buku jero kwa mwezi!

Sasa nawauliza hawa wataalam wetu wa kodi wametumia kigezo gani cha kutuadhibu wenye ghorofa? Kujenga ghorofa ni ishara ya utajiri na nyumba ya chini ni umaskini?

Nina mashaka na mfumo wa elimu wetu, huenda unazalisha wajinga zaidi
KWA CCM HII UTALIPA UTAKE AU USITAKE NA KAMA HUTAKI BEBA GHOROFA LAKO PELEKA BURUNDI
 
Mimi nina Kajumba kangu huku uswahilini, kwa sababu ya ufinyu wa eneo nilijiongeza nikawekwa kaghorofa. Sasa serikali inanitaka nilipe elfu 15 kila mwezi. Yupo jirani yangu aliwanunua watu na kupata eneo kubwa, kuliwekea Uzio na kushusha mjengo wa kisasa wa nguvu.

Thamani ya jengo la jirani inaweza kuwa mara tano ya kaghorofa kangu, yeye atakuwa analipa buku jero kwa mwezi!

Sasa nawauliza hawa wataalam wetu wa kodi wametumia kigezo gani cha kutuadhibu wenye ghorofa? Kujenga ghorofa ni ishara ya utajiri na nyumba ya chini ni umaskini?

Nina mashaka na mfumo wa elimu wetu, huenda unazalisha wajinga zaidi
Kuna kitu labda haujakielewa sababu serikali haijakiweka wazi. Ni hivi, wewe mwenye kaghorofa unalipishwa zaidi sababu una access ya kuwaona jirani zako bure wakiwa wanaoga/wanajisaidia au kwenye faragha zao nyingine nje pasipo na paa.
So hicho ndicho unachokilipia
 
Na wanaohusika na ukadiriaji wa Kodi za majengo ni wasomi tena wengine ni maprofesa
Kwa mfumo wetu wa Tanzania mtu kuwa tajiri ni dhambi si sawa. Utakuja kiongozi anajinadi mimi n mtoto wa masikini inabidi wabadirike. Kuhusu maprofesa ile kesi ya madini imeonyesha nao ni weupe tu vichwani.
Kuhusu kodi BASI ANGALAO WANGETUWEKEA MAZINGIRA MAZURI mtu akijenga kagorofa awe na kabarabara ka lami, security na miundo mbinu mingine kama mtandao wa gas, maji na umeme wa uhakika.
 
Mimi nina Kajumba kangu huku uswahilini, kwa sababu ya ufinyu wa eneo nilijiongeza nikawekwa kaghorofa. Sasa serikali inanitaka nilipe elfu 15 kila mwezi. Yupo jirani yangu aliwanunua watu na kupata eneo kubwa, kuliwekea Uzio na kushusha mjengo wa kisasa wa nguvu.

Thamani ya jengo la jirani inaweza kuwa mara tano ya kaghorofa kangu, yeye atakuwa analipa buku jero kwa mwezi!

Sasa nawauliza hawa wataalam wetu wa kodi wametumia kigezo gani cha kutuadhibu wenye ghorofa? Kujenga ghorofa ni ishara ya utajiri na nyumba ya chini ni umaskini?

Nina mashaka na mfumo wa elimu wetu, huenda unazalisha wajinga zaidi
sheria zipo na hazijafutwa sema PhD feki za uchumi ndio zinatusumbua
 
Mimi nina Kajumba kangu huku uswahilini, kwa sababu ya ufinyu wa eneo nilijiongeza nikawekwa kaghorofa. Sasa serikali inanitaka nilipe elfu 15 kila mwezi. Yupo jirani yangu aliwanunua watu na kupata eneo kubwa, kuliwekea Uzio na kushusha mjengo wa kisasa wa nguvu.

Thamani ya jengo la jirani inaweza kuwa mara tano ya kaghorofa kangu, yeye atakuwa analipa buku jero kwa mwezi!

Sasa nawauliza hawa wataalam wetu wa kodi wametumia kigezo gani cha kutuadhibu wenye ghorofa? Kujenga ghorofa ni ishara ya utajiri na nyumba ya chini ni umaskini?

Nina mashaka na mfumo wa elimu wetu, huenda unazalisha wajinga zaidi
Mkuu hawa watawala walishatufanya mazuzu, wamehamisha tozo ya miamala wakaileta kwenye kodi ya majengo. Tusubiri kodi zingine zaidi kwa hasira za kukataliwa mission yao ya DP World
 
Back
Top Bottom