Kodi ya mapato kwa magari ya mizigo

Kodi ya mapato kwa magari ya mizigo

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2012
Posts
2,025
Reaction score
1,270
Habari wana JF,

Kuna gari langu la Suzuki Carry niliagiza toka Japani mwezi May mwaka huu na nikaliweka barabarani baada ya kwisha kulipia kodi zote. Hivi majuzi gari langu lilikamatwa na watu wa TRA wakishirikiana na Majembe Auction (Wazee wa kazi) wakidai sijalikatia kodi ya mapato. Wazee wa Majembe waliweka katika yard yao na siku iliyofuata nilireport TRA Chang'ombe kupewa maelezo ya kina ambapo niliambiwa natakiwa nilipe shs 450,000 kama kodi ya mapato ya gari na dereva kwa mwaka.Baada ya mvutano mrefu nililipa kodi husika katika Bank wanayotumia na kuwaletea nakala ya stakabadhi husika halafu wakatoa notice ya gari langu kuachiwa. Katika hii Scenario naomba mnitoe ushamba kidogo kwa kunijibia maswali yafuatayo:-

1. Hii ya kodi mpya ya mapato mbona nijawahi kuiona au kuisikia kupitia Government Notice (Gazeti)
2. Hivi mtu akiwa na Suzuri carry yake nyumbani kwa ajili ya shughuli ya kifamilia anatakiwaje kulipa kodi ya mapato?
3. Kama hii kodi tajwa ni halali, je kuna yeyote aliye na ufahamu mpana utufumbue macho wengi wetu?
4. Idd mbaraka kwa wahusika wote

Nawakilisha
 
Ni wizi mtupu wa serikali ya ccm,hata kama gari yako iko kwenye mawe kwa mwaka mmoja ukija irusisha barabarani watataka ulipie kile kipindi ambacho gari ilikuwa juu ya mawe
 
Mzalendo_Mkweli
Hata kama una Carry ya nyumbani unalipia

Wanakuambia kwamba inazalisha,maana kama una Carry huwezi kutumia kwenda kazini au Day out.Lazima utakuwa na kazi nayo inayokuzalishia,kama kubeba majani ya ng`ombe,dukani nk

Wa sijui kitaalam wanaita Utility Vehicles,na ndio maana TRA wanakupa Utility Card kulingana na Tani za gari lako.

Ila cha kushangaza ukienda Halmashauri wao hii Kodi hawaijui kabisaa,maana wakati unafanya usajili sehem zote,unaambia hapo umekamilisha,ukiingia njiani ndio unakutana na hao Jamaa.
Sasa kwa wale wachimba mchanga naona ndio wanakazi kubwa,maana kule Halmashauri husika zinawacharge ukija TRA pia wanacharge.
 
Back
Top Bottom