MR TOXIC
Senior Member
- Jun 4, 2019
- 190
- 525
Ni wiki chache tu tangu serikali ianzishe kodi ya miamala ya simu kwa madai kwamba mapato yatakayotokana na tozo hizo yataenda kufungua barabara za mjini na vijijini.
Lakini juzi, waziri huyo huyo aliyetuaminisha kwamba barabara zitajengwa kwa kodi inayotokana na tozo ya miamala ya simu ameziagiza halmashauri zote kutenga bajeti kupitia mapato ya ndani kwaajili ya ujenzi wa barabara.
Serikali hakuishia kuahidi barabara bali pia kupitia waziri wa fedha alisema wana mpango wa 'kuinject' uchumi au kuweka mzunguko wa fedha kwa watu lakini matokeo yake tunaona mfumko wa bei za bidhaa ikiwemo mafuta, gesi, mbolea n.k vikizidi kupaa juu.
Sasa tujiulize,
Kama barabara zinajengwa kwa mapato ya ndani ya halmashauri na mzunguko wa fedha bado ni mdogo mtaani, je kodi ya miamala ya simu inayokusanywa kwa kuumiza wananchi inakwenda wapi?