Kodi ya Pango: TRA yatoa ufafanuzi kuhusiana na kodi ya pango

Kodi ya Pango: TRA yatoa ufafanuzi kuhusiana na kodi ya pango

Jenga yako mkuu maana kuna kodi mbili analipa mwenye nyumba moja ni ardhi nyingine nu majengo, sasa hii nyingine hapana
Mkuu any business deal unatakiwa kulipia kodi acha kulalamika.

Hizi pesa kwa asili ni za serikali sio zako. Rejea habari hii ambayo familia ilifikiri ndugu yao ni tajiri sana na anastahili kuzikwa na pesa anazomiliki;

"Wanasheria nchini Uganda wameamua kuifikisha familia ya Ivan Mahakamani kwa makosa ya kuzika pesa halali za Jamhuri ya Uganda katika kaburi la ndugu yao Ivan. Kwa nchi yoyote kitendo hicho hakikubaliki kwani pesa hizo zingeweza kutumika katika shughuli zingine na kukuza uchumi wa nchi"

Kama kujenga nyumba yangu hatua inaendelea, haina shaka. Nataka tu tujaribu kuwa chanya kwa baadhi ya Mambo ya nchi yetu, mengi ni mazuri labda tuseme wengi hatuna imani na matumizi ya watu wetu hapo juu but let us "trust the process"
 
chonde chonde Serikali na watu wako, tumia hizi pesa zetu vizuri kwa nidhamu kubwa, kinyume na hapo machozi yetu yatawang'oa kwenye hivyo viti.
Mmmmh!.
 
Uzuri sisi waislamu kila muislamu ni ndugu yako technically ntakua nakaa nyumba za wajomba zangu tu
 
Hakuna kodi inayoitwa ya kiwanja, kuna kodi ya ardhi ambayo inakusanywa na wizara ya ardhi na ni kwa kiwanja kilichopimwa tu.halafu hiyo inayolipiwa kuoitia luku ni kodi ya majengo(property tax) hii tena ni kidi ya zuio(withholding tax)ni 10% ya kodi ya upangishaji anatakiwa kulipa mwenye nyumba kupitia kwa mpangaji.
Yaani kama kwa mwaka unamlipa mwenye nyumba laki 6, asilimia 10 yake ambayo ni 60, 000 unatakiwa ukailipe TRA, na mwenye nyumba umpe 540, 000.inayobakia.
je unawezekanika kumpa mwenye nyumba Kodi pungufu? unadhan utakaye umia ni mpangaji ama mwenye nyumba yake ama serekalii?
 
Serikali itoe tamko kuhusu wenye nyumba kuongeza kodi ya nyumba kutokana na uamzi huu. Ni marufuku kupandisha bei, la sivyo tutaumia sisi wapangaji wakati nyie fahari wawili mkipigana.

Vinginevyo ni uamzi mzuri mno. Binafsi ilikuwa haingii akilini kuona mwenye nyumba anapokea kitita chote bila kukatwa kodi.

Japo kwakweli chonde chonde Serikali na watu wako, tumia hizi pesa zetu vizuri kwa nidhamu kubwa, kinyume na hapo machozi yetu yatawang'oa kwenye hivyo viti. Narudia tena, tunataka tuone maendeleo kutokana na tozo zote hizo, NIMEMALIZA.
Kwani ni Mara ngapi Kuna tozo na makato mbali mbali na kulia ushalia sana na bado watu wanapanda vyeo? laana km hizi hazifikagi kwasababu ni laana zinazotokana na uzembe wa wahusika kukubali kuburuzwa
 
Kodi ya ardhi hata usipopangisha nyumba yako utalipa tu

Unalipa kodi ya ardhi kwa sababu hiyo ardhi siyo ya kwako bali umepangishwa tu.

Ukijenga Nyumba ukaifanya kuwa ya biashara maana yake utapata kipato, why usilipe kodi ya pango?
Lazima ulipe withholding tax
Tatizo wabongo tumezoea kuishi kimazoea

Ova
 
je unawezekanika kumpa mwenye nyumba Kodi pungufu? unadhan utakaye umia ni mpangaji ama mwenye nyumba yake ama serekalii?
Hapo kunategemea na uelewa wa mwenye nyumba mbona wafanya biashara wengi tumekuwa tukifanya hivyo na mwenye nyumba anaelewa?mnao liona geni ni nyie ambao hamjawahi kupanga sehemu za biashara hasa kwenye miji mikubwa, zoezi hili litakuwa gumu kwenye upangishaji wa nyumba za kuishi, lakini kwenye fremu za biashara ni rahisi tu, kwani hupati tin number bila kupeleka mkataba wa pango, sasa mwenye nyumba utakuwa huna akili ukatae, yaani upangishe fremu kwa 50, 000 , kukatwa kodi ya 5000 uone nyingi?!!
 
Hii ni kwa wale pato linaloanzia 500000tsh kwa mwaka...na ukweli kila baishara inayofanyika inabidi kulipa kodi tu inderct au direct way sa uyo bibi unayemsema sizani kama nyumba anayopangisha itakua inafikia kiwango icho kwa kwa mwaka.
 
Mkuu any business deal unatakiwa kulipia kodi acha kulalamika.

Hizi pesa kwa asili ni za serikali sio zako. Rejea habari hii ambayo familia ilifikiri ndugu yao ni tajiri sana na anastahili kuzikwa na pesa anazomiliki;

"Wanasheria nchini Uganda wameamua kuifikisha familia ya Ivan Mahakamani kwa makosa ya kuzika pesa halali za Jamhuri ya Uganda katika kaburi la ndugu yao Ivan. Kwa nchi yoyote kitendo hicho hakikubaliki kwani pesa hizo zingeweza kutumika katika shughuli zingine na kukuza uchumi wa nchi"

Kama kujenga nyumba yangu hatua inaendelea, haina shaka. Nataka tu tujaribu kuwa chanya kwa baadhi ya Mambo ya nchi yetu, mengi ni mazuri labda tuseme wengi hatuna imani na matumizi ya watu wetu hapo juu but let us "trust the process"
Umetoa mfano tofauti kuzika pesa au kuchana pesa yako ni kosa la Jamhuri mkuu hili nalo linahitaji Elimu ya Sensa..
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] wapangaji wajipange
Tutajipanga vipi wakati hutu tuhela tudogo tunadunduliza tunampa mwenye nyumba kiasi chake cha kodi bado na serikali nae anataka kodi,tutajenga kweli?

Huko tuendako si kuzuri,lakini ninachoamini kwa hili watafeli tu,tatizo nchi hii hupenda mambo ambayo kwa hali ya nchi hasa kiuchumi hatujafikia
Serikali umeshindwa kutoa ajira kwa raia wako halafu bado unawadai makodi ya ajabu
Majority ya watanzania ni watu masikini wenye majumba wachache wapangaji wengi sasa ngoja tuone kama sisi kwa mamilioni watatuweka rumande ipi tuenee.

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Hahaha, yani TRA wanachekesha sana, kwa hiyo wamejiona wametoa ufafanuzi wa kina, kwamba kodi sio mpya ila, “WAMETANUA WIGO”. Suala liko hapo, kwanini watanue!?

Mbona Watanzania malalamiko yao hayapo kwenye kodi ni ya zamani au mpya! Na wanatumia nguvu nyingi kuaminisha kwamba ikilipwa na wenyenyumba basi wapangaji haitawagusa, hawawazi kwamba kodi za vyumba na nyumba zitapanda!
 
Kwani ni Mara ngapi Kuna tozo na makato mbali mbali na kulia ushalia sana na bado watu wanapanda vyeo? laana km hizi hazifikagi kwasababu ni laana zinazotokana na uzembe wa wahusika kukubali kuburuzwa
Hizi laana zinafika sana mkuu, mbona unakuwa mwepesi kusahau historia? Kama wewe ni kiongozi usicheze na hizi laana, tutakusahau kabisa kama ulikuwa kwenye uso wa dunia.

Ogopa sana sauti ya wengi huwa ni sauti ya Mungu.

Makaburi yamebeba watu wengi waliodhani ulimwengu hautaendelea bila wao! Wewe endelea kujitutumua[emoji2097][emoji2097]
 
Serikali itoe tamko kuhusu wenye nyumba kuongeza kodi ya nyumba kutokana na uamzi huu. Ni marufuku kupandisha bei, la sivyo tutaumia sisi wapangaji wakati nyie fahari wawili mkipigana.

Vinginevyo ni uamzi mzuri mno. Binafsi ilikuwa haingii akilini kuona mwenye nyumba anapokea kitita chote bila kukatwa kodi.

Japo kwakweli chonde chonde Serikali na watu wako, tumia hizi pesa zetu vizuri kwa nidhamu kubwa, kinyume na hapo machozi yetu yatawang'oa kwenye hivyo viti. Narudia tena, tunataka tuone maendeleo kutokana na tozo zote hizo, NIMEMALIZA.
Natamani ungekuwa unavyotoa kauli hiyo unatizamana uso kwa uso na mama[emoji23][emoji23]
 
serikali ni watu na TRA ni taasisi ndani ya serikali inabidi pia waeleze mchakato mzima wa pesa zinavyo tumika za kodi kwa matangazo hii itasaidia watu kulipa bila kukimbia kimbia .
Tunajua kwamba moja ya matumizi ni kununua V8 kwa gharama ya zaidi ya bilioni 500...
 
Umetoa mfano tofauti kuzika pesa au kuchana pesa yako ni kosa la Jamhuri mkuu hili nalo linahitaji Elimu ya Sensa..
Logic ni kwamba hizi pesa hizi tunazomiliki ni za Jamhuri, wala sio zako sio zangu na si za Mwigulu.

Kwenye huo mfano hujawaza kwanini ukizikwa na nguo zako zote - no problem? Sijajua kuhusu kuzikwa na magari yako.

Kwahiyo tuache kukumbatia pesa saaana sio zetu, mpe kaisari.
 
Back
Top Bottom