Kodi ya RAV 4 ya 2005

darling-tone

Member
Joined
Apr 24, 2013
Posts
60
Reaction score
11
Assalam aleykum, bwana Yesu asifiwe.

Wanajamvi ninaomba msaada kwa anayejua kodi itakayokatwa na watu wa TRA kama ninaingiza gari ya dola 6000 nje ya gharama za usafiri ya mwaka 2005. Nikiweka gharama za usafiri ni kama dola 7900's. Nihabarisheni na gharama zingine nitakazoingia mbali na kodi. Ni mara yangu ya kwanza kufanya hizi transaction mwenyewe hivyo ninaomba uzoefu wenu wanajamvi.

Ninaamini kwenye wengi hapaharibiki neno.

Asanteni.
 
binafsi ningependa kujua pia habare hii ila wenye jamvi wamekaa kimyaaaaaaaaaaaaaaaaa mukuje basi mumudadavulie mleta uzi kuhusu haya ili nasie tufaudu.
 

...Ingia website ya TRA, download tax calculator, kule kuna bei ya gari zote na formular ya kupata cost za ushuru kwa hilo gari unalohitaji.

...kwa hesabu za haraka MPAKA GARI INAINGIA BARABARA ZA TZ, NA KUANZA KUKATA MITAA BILA KUDAIWA KITU CHOCHOTE, fanya mara mbili ya bei unayonunulia kule Japan (approximately)
 
........
Mimi pia.....
Tuwasubiri majemedari

...au ingia huku...
Welcome to GariYangu.Com
Want to know your car import tax? Use this car import tax calculator Old CIF
based calculator is also available · Get A Clearing Agent Get a clearing agent
with...
===

GariYangu.ComBefore you import your dream car , read this!
Want to know your car import tax?
Use this car import tax calculator
===
http://www.gariyangu.com/
 
Kwanza kabisa Tra hawatataka kujua ilo gari umenunua kiasi gani,watakuja na makisio yao,Rav 4 ya 2005 kwa CIF ya $ 7900 ni ndogo sana wao wanaweza sema CIF ni $11000 na ndio wakapigia hesabu,hivyo nakushauri 9ml uwe nayo itatosha mpaka na chai ya mkaguzi pale Bandarini.Kama una agent mzuri mpe namba tano za mwanzo za chasis namba ya ilo gari atakupa makisio mazuri zaidi,maana si Rav 4 zote za 2005 zina tax inayofanana
 

Umejibu vyema. nilishaingiza mpendwa. CIF yao ni nyingine kabisa tofauti ya uliyonunulia. kwa ufupi kama mtu anaagiza gari japan ni vyema hela anayonunulia kule aidabo mara mbili na zaidi.
 
Umejibu vyema. nilishaingiza mpendwa. CIF yao ni nyingine kabisa tofauti ya uliyonunulia. kwa ufupi kama mtu anaagiza gari japan ni vyema hela anayonunulia kule aidabo mara mbili na zaidi.


Au aidabo mara tatu kabisa amalize mchezo.
 

Utalipa kodi ya dola 1701 ukitaka kufanya hesabu nenda download hapa utapata sheet ya excel ingiza gharama ya hiyo gari mengine yatakupa majibu yenyewe.

Tanzania Revenue Authority - Calculators & tools
 
Umejibu vyema. nilishaingiza mpendwa. CIF yao ni nyingine kabisa tofauti ya uliyonunulia. kwa ufupi kama mtu anaagiza gari japan ni vyema hela anayonunulia kule aidabo mara mbili na zaidi.

Kwanini TRA wana toza kodi ndefu hivyo, hii inakua kama kukomoana vile. Au kuna mchezo mchafu wanaucheza na wamiliki wa yard za kuuza magari, kwa ku-discourage watu/mtu mmoja mmoja kujiagizia gari ili wamiliki wa yard waweze piga hela. (Just Saying:music::music::music🙂
 
Umejibu vyema. nilishaingiza mpendwa. CIF yao ni nyingine kabisa tofauti ya uliyonunulia. kwa ufupi kama mtu anaagiza gari japan ni vyema hela anayonunulia kule aidabo mara mbili na zaidi.

Vp ulilipia sh.ngapi?
 
Au aidabo mara tatu kabisa amalize mchezo.

Hahahahaaa, au aidabo mara nne kabisa ili kukamilisha na mafuta ya miezi mitatu...lol!
Suala siyo kudabo, ingia kwenye website ya TRA kuna kikokotoo kitakupa mwanga, ukiona vipi wasiliana na agent umpe VIN au piga huduma kwa wateja, unapata figure inayoeleweka!
 
[TABLE="width: 585"]
[TR]
[TD="colspan: 7"]Motor vehicle with more than 1000cc but not exceeding 2000cc[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 7"]Example of vehicles: Toyota Mark II Model GX110, Toyota Corolla, Subaru forester, RAV4,Pajero Junior (io)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 7"]GUIDELINE SUBJECT TO VERIFICATION[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Current Retail Selling Price[/TD]
[TD] 60,844[/TD]
[TD="colspan: 4"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Depreciation[/TD]
[TD] 70%[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Freight[/TD]
[TD] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Customs value[/TD]
[TD] 9,429[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]FOB Value[/TD]
[TD] 9,429[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Import Duty 25%[/TD]
[TD] 2,357[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Excise Base[/TD]
[TD] 11,786[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Excise Duty 5%[/TD]
[TD] 589[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]VAT Base[/TD]
[TD] 12,375[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]VAT 18%[/TD]
[TD] 2,228[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Total Taxes[/TD]
[TD] 5,174[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Total Taxes in TSHs[/TD]
[TD] 8,381,799[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 3"] [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Vp ulilipia sh.ngapi?

Gari ya 2008, bei yake ilikuwa M. 18 kodi M.13 jumlisha na mengine yote mpaka kuwa barabarani ilifika kama M. 38 hivi. Jamaa hawaangalii bei ya japan. Jamaa wana system yao ambayo wanakwambia hawaangalii CIF , ni kama wanakomoa vile.
 

Nilishangaa hata mimi. HADI GARI YAKO IWE BARABARAI JITAHIDI UJIANDAE KWA HELA NYINGINE KAMA ILE ULIYOAGIZIA KULE (hiyo unayoandaa ni kodi, agency fee, sijui malipo gani kule farion (hapa itategemea unatolea geti gani, kama utachelewa kuprocess TIN number jua kuna storage charges na mengine kama watakavyokuambia). System ipo kwa ajili ya calculation ila ukiitegemea hyo unaweza kuacha gari yako pale bandarini hivi hivi unaiona. nasema hivi kulingana na utaratibu wao wa calculation ambao hasa unaangalia gari (na kutafuta market price yao) na sio CIF ya japan.
 
@lucky sabasaba jaribu kuwaelewesha hawa.... unaweza jiridhikia na CIF yako ya hukooo ulikonunulia ila yai likitua bandari ya dsm ukaona mahesabu yanavyonyanyuliwa. TRA ni majangili a.k.a wezi asee
 
Wakuu mimi nina swali juu ya hili.

Hili gari kwa vyovyote litakuwa na umri unaozidi miaka 8,je halitatozwa kodi ya uchakavu?Hii ni kwa sababu niliona kwenye budget iliyopita kuna kipengele kilitumika kupunguza umri wa kutozwa kodi ya uchakavu toka miaka 10 hadi 8.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…