Kodi ya uagizaji gari Japan kuja Tanzania unatisha. Land cruiser Prado bei TZS 40,638,290 (hadi Mwanza via DSM). Kodi + gharama zingine 42,060,235!!

Uzima Tele

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2023
Posts
1,270
Reaction score
2,822
Mfumo wa kodi ya uagizaji gari (used abroad) toka nje hususani Japan kuingia Tanzania unatisha na kushangaza sana...

Mathalani hivi inawezekanaje kodi na gharama zingine pale bandarini ziwe kubwa kuliko bei ya gari yenyewe? Msingi wa kutoza kodi kwa jinsi hii UNAKUWA ni nini eti..?

Nimeagiza gari yangu [Land Cruiser Prado TRJ150 ya mwaka 2011 toka Japan juzi kati hapa kupitia kampuni ya Be Forward nipokelekee Mwanza kupitia bandari ya DSM..

Kodi na gharama zingine kupitia TRA yetu ni kubwa kuliko bei niliyonunulia na kuisafirisha hadi Mwanza...!!

Gari yenyewe hiyo ☝️☝️☝️☝️pamoja na total price yake [C&F Mwanza via bandari ya DSM]

Hizo☝️☝️☝️☝️ ndo kodi za TRA. Ni kubwa kuliko bei ya gari yenyewe. Kodi inatozwa hadi kwenye ZERO income...!!
 
Wanakuja wajuaji wakupe muongozo. Kiufupi kama unaweza kununua punda ww nunua akuzungushe mjini magari tuyaache tu.
Mkuu yaani TRA ukinunua gari Wana wanakuja wakuuzie Tena wewe
 
Vitu vya kupunguza haya makali ya maisha wanawapa wajomba wa Oman kwa kisingizio cha uwekezaji
 
Serikali ya majizi huweka kodi umiza kwa raia lakini kwao kila kitu kina msamaha wa kodi. Wakiagiza gari haitozwi kodi, kuna wengine hadi mishahara yao ya kujipimia haina paye ila mshahara kibaba wa mwalimu una paye na makato mengine kibao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…