Kodi ya uchakavu imenichanganya

screpa

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2015
Posts
10,857
Reaction score
15,866
Wakuu nimekuwa confused kidogo hapa, nilihitaji kuchukua gari hii ila kikokotozi cha TRA kimenishangaza, nilihitaji kuchukua Toyota Allex ya 2005 ila nimeshangaa kuona gharama ya uchakavu ya 2005 ni kubwa kuliko matoleo yake ya nyuma ya mfano huo 2003, inakuwaje hii? Nachoelewa mimi miaka ya jinsi inavyokuwa imepita mingi ndio gharama ya uchakavu inavyoongezeka. Hapa nimeshindwa kuelewa kwanini imekuwa kinyume LEGE, mshana jr na wataalam wengine


2005



2003


2006
 
Ingawa picha zako hazionekani vyema, lkn kwa nijuavyo mimi ni kuwa kodi zote ikiwemo hiyo ya uchakavu huwa inakokotolewa kutokana na thamani ya gari!

Gari linavyozidi kuzeeka ndo thamani yake inazidi kushuka mfano gari ya 2003 inaweza kuwa $2500 na ya 2005 ikawa labda $3500. Thamani za magari wanazijua wao TRA. Kwa mfano kama kodi ya uchakavu ni 10% then gari ya 2003 itakuwa na kodi ya uchakavu ya $250 wakati ile ya 2005 itakuwa na $350.
 
Ok, but nachoshangaa mbona kodi ya uchakavu ya 2006 ni ndogo kuliko 2005, na kodi ya 2005 ni kubwa kuliko 2004 na 2006?
 
Mmh nahitaji muda kwenye hili naona kama sio kawaida
 
Ok, but nachoshangaa mbona kodi ya uchakavu ya 2006 ni ndogo kuliko 2005, na kodi ya 2005 ni kubwa kuliko 2004 na 2006?

Gari ya 2005 kushuka chini uchakavu ni 30%, gari ya 2006-2008 uchakavu ni 15% na gari ya 2009-to date hazina uchavu. Maelezo mengine ni kama mdau alivyokuambia hapo juu kwamba thaman ya gari huongezeka kadili inavyokuwa mpya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…