DENLSON
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 949
- 1,260
Leo tarehe 15 Julai 2021, Selikari isiyopenda kukusanya kodi ya dhulma kupitia wizara yake ya fedha imeanza rasmi kutekeleza makato ya kodi ya kizalendo inayokatwa moja kwa moja katika miamala ya kifedha ya mitandao ya simu. Sina tatizo na kodi hiyo ila tuna mengi ya kujadili kuhusiana na ukusanywaji, matumizi yake na walengwa wa kodi hii.
1. UKUSANYWAJI WA KODI YA KIZALENDO:
BENKI PIA ZIWE NA MAKATO: Kwakuwa kodi hii imepewa jina la Kodi ya kizalendo basi inatakiwa kubeba maana halisi ya udhalendo kwa maana ikatwe kwa Watanzania wote na sio watu wachache kwa sasa bado haibebi maana halisi kwa sababu kupitia miamala ya simu maana yake wanaolipa kodi hii ni watu wa kipato cha kati na kipato cha chini tu. Hii kodi haitowagusa wafanyabiashara wakubwa au matajiri kwakuwa hao fedha zao hazipiti kwenye mitandao ya simu wao fedha zao hupita benki au wanalipa/pwa cash. Hivyo kuleta maana hii kodi isiishie katika mitandao ya simu tu iende mpaka benki mtu akitoa fedha au kuweka akatwe sawasawa na viwango vya simu.
KILA JIMBO, WILAYA, MKOA NA KANDA IJULIKANE MAPATO YAKE: Kwa kuwa hii ni kodi inayolenga kuimarisha miundo mbinu ya vijijini basi kodi hizo ni bora zikakusanywa katika uwiano wa majimbo, wilaya, mikoa au kanda ili kuweka mgawanyo sahihi katika kupeleka miundo mbinu ili kila anayekatwa aone ikifanya kazi mahali husika. mfano iwepo namna kwamba kodi inayotozwa Mbeya ijenge miundombinu ya vijij vya Mbeya kwanza ziada ndio iende sehemu nyingine ili yasitokee yale ya Chato kupewa kipaumbele huku kodi wanakatwa watanzania wote.
2. MATUMIZI YA KODI YA KIZALENDO
Kodi hi itumike kuimarisha huduma za dharura: Tunajenga miundo mbinu mingi lakini huwa hatufanyi risk analysis inayoweza kutokea kutokana na uwepo w hiyo miundo mbinu. Mfano: Ujenzi wa barabara njia nane Kibaha-Ubungo inaweza kuwa chanzo cha ongezeko la ajali hivyo basi ni vyema kipaumbele kikawekwa katika uimarishaji katika utoaji wa huduma za dharura au kununua magari ya ambulance za kutosha na kuimarisha utoaji wa huduma za dharura zinapohitajika hii iende sambama na mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere na SGR angalau kwenye kila 50km kuwe na kituo cha kutolea huduma za dharura chenye gari za wagonjwa.
Kodi itumike katika vitu tangible: Hii kodi itumike shehemu itakayoonekana na kuleta impact kwa jamii husika, hatutegemi kusikia watu walipane posho kupitia hela za hii kodi, tunataka kuona barabara, shule, zahanati na miundo mbinu ya umwagiliaji ikijengwa kupitia kodi hii. Sio mje mseme tunapeleka umeme ikiwa tunajua kuna fesha zinakatwa kwa ajirli ya umeme katika mafuta.
Mwisho nashauri makusanyo ya kodi hii yawekwe wazi kwa kila jimbo, wilaya, mkoa na kanda ili ijulikane wazi kuwa fedha inayopatikana ni kiasi gani na matumizi yake ni yapi.