Kodi ya Watengeneza Maudhui Mtandaoni: Ubunifu unakufa taratibu

Ni Desemba 16, 2025, Kampuni ya Meta ilithibitisha rasmi kupokea ombi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) la kukata kodi ya asilimia 5 kwa kila malipo yanayolipwa kwa Watengeneza Maudhui (Content Creators) wanaoishi Tanzania. Utekelezaji wa mfumo huu unaanza Desemba 21, 2025, hatua inayozua mjadala mpana kuhusu mustakabali wa ubunifu wa kidijitali nchini.
View attachment 3516446
Kwa mujibu wa utaratibu huu, mtengeneza maudhui aliyepaswa kulipwa TSh milioni mbili atalazimika kukabidhi TSh 100,000 kama kodi, bila kujali ukubwa wake au changamoto alizopitia kufikia kiwango hicho. Makato haya yanahusu mapato yanayotokana na programu za Facebook kama Stars, Subscriptions, Bonuses na Content Monetisation Beta, pamoja na Instagram kupitia Gifts, Subscriptions na Bonuses.
View attachment 3516447
Meta inajiunga na YouTube, ambayo tayari imeanza makato ya aina hii tangu Julai 2025. Hata hivyo, swali kubwa linalobaki ni: Je mfumo huu unahamasisha ubunifu au unauua kabsa?
View attachment 3516448
Kwa uhalisia, kodi hii inaumiza zaidi watengeneza maudhui wadogo—wale wanaojitahidi kukuza akaunti zao, kununua vifaa, intaneti na muda. Asilimia 5 kwa mkubwa na mdogo ni sawa kisheria, lakini kiuchumi ni pengo kubwa. Mbaya zaidi, makato haya yanakuja juu ya mlolongo mrefu wa kodi zingine: vocha, miamala ya simu, benki na huduma za mtandao ambazo poa TRA huchukua kodi.
View attachment 3516449
Badala ya kujenga mazingira rafiki ya uchumi wa kidijitali, hatua hii inaonekana kama kukata tamaa ya ubunifu kabla haujakua. TRA inaonekana mahiri sana katika kubuni njia za kukusanya kodi, lakini dhaifu katika kueleza wazi matumizi ya fedha hizo kwa maendeleo ya wananchi.
View attachment 3516446
Swali la msingi linabaki: Je Tanzania inataka kukuza uchumi wa ubunifu au kuudhibiti mpaka ufe? Kama sera hazitatazamwa upya, huenda ndoto ya vijana wengi wa kujitegemea kupitia maudhui ya mtandaoni ikabaki kuwa hadithi tu. Wataalamu wenu wa masuala ya ushauri wa kodi wanawashauri vitu gani?
watoze kodi kila account iliopo mitandaoni
 
Safi sana
 
Hiyo ni sawa kabisa.
Asilimia 5% ni reasonable price.
Muhimu kusiwe na mambo sijui ya leseni isipokuwa kwa mambo ya kitaalamu.
Not reasonable kwa angle ya serikali kupiga pin mitandao ya kijamii. Haiwezekani utake kuchukua 5% unapiga pin twitter au JF au Tiktok; hao creators sasa wataonesha wapi sanaa zao?
 
WEWE UKIZIBIWA NJIA MOJA UNAHIRISHA SAFARI NA SIO KUANGALIA NJIA MBADALA

DON'T BE THE WEAK PERSON
 
I am kind and not weak/soft. Rejelea principles of good tax system. Yaani ufungie mitandao ya kijamii halafu hapo hapo unawatoza kodi ya 5% ya maudhui wanayoyatengeneza? It is counterproductive and not sensible at all.
 
Kila anaeingiza kipato lazima alipe kodi. Tunatakiwa kuishinikiza serikali kutumia kpdi zetu vizuri sio kununua silaha na kuwalipa watu watuue.
Wabunge wanalipa kodi?
Kwa nini wilaya moja iwe na DC, DAS, DED na Mwenyekiti wa Halmashauri?
Kwa nini tunaendelea kuwa na Wabunge wa viti maalumu mpaka leo wakati usawa wa kijinsia umeshapatikana kikamilifu?
Kwa nini tuna nafasi ya waziri mkuu na makamu wa Rais?
Kwa nini wenza wa watawala wanalipwa kwa kodi zetu kwa sababu tu wameolewa au wameoa watawala??
 
Kuna prado new model za serikali watu wanazunguka nazo tu mtaani leo unaikuta wameweka na B kesho A, tuendelee kulipa kodi kwa bidii. Kuna mwamba hapo kale alisema "serikali haina shamba"
 
Back
Top Bottom