Kodi za kwenye mafuta ziangaliwe upya

Kodi za kwenye mafuta ziangaliwe upya

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Asikudanganye MTU hata kama ukiongeza mshahara lakini ukaongeza bei ya mafuta ni kama umechukua ulichoongeza.

Nani humu JF anazifahamu kodi zilizomo kwenye mafuta ya petroli na mafuta ya kula atujuze?

Hali za wananchi bila kujali vyama vya siasa zinatia mashaka, kiuhalisia hawatofautiani sana na Kuku wa kienyeji kujitafutia wenyewe dawa wakiumwa, masoko ya mazao yao wakivuna, madawati shuleni, mabweni kwa watoto wao, barabaara, maji ya kunywa, vitaa vya sola wapate mwanga na mambo mengi.

Maendeleo wanayataka lakini hebu wahusika angalieni kodi zisizo na ulazima kwenye maisha yao zitazosaidia kuwapatia ahueni watanzNia hawa wanaoimba hiyenahiyena kama mazuzu bila kujali wamekula na kuvaa nini mwilini na miguuni.
 
Ni bajeti ya mchumi wa daraja la kwanza. Haija wahi kutokea bajeti ya ajabu kama hii. Tangu hii nchi ipate uhuru.
 
Mafuta yanapita Bandarini hapa lakini nchi jirani yanauzwa nafuu.Waliomipakani Wana bahati wao wanavuka tu boda wanajaza fully tank wanapiga misele tu

IMG-20210711-WA0026.jpg
 
Wananchi hatuwezi kukubali kukandamizwa na Serikali kama sisi ni wajinga.
 
Tuache uchadema na uccm na uact na unccr. Tunaangamia wote kwenye tanuru moja lisilobagua chama, kabila wala dini ya mtu. Kama vyama vitatupofusha fikra zetu tukaacha kuifikiria Leo yetu basi kesho yetu itakuwa ya taabu sana.

Ni kweli kuwa siku hizi hakuna wahisani wa kuja kutuketea maji na Barbara lakini ni kweli pia tuna kodi nyingi na matumizi mengi ya kifisadi kama vile ruzuku za vyama, kununua wanasiasa na wizi kwenye manunuzi.
 
Back
Top Bottom