Kodi za Mapato: Kabla hatujawaza kuzidi kukamuana, tuangalie kuziba Pakacha

Kodi za Mapato: Kabla hatujawaza kuzidi kukamuana, tuangalie kuziba Pakacha

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Kuna Notion kwamba Watu hawalipi Kodi, na bila kuongeza vyanzo kwa kuwakamua zaidi Nchi haiwezi kuendelea...

Kwanza kabisa sio kweli kwamba watu hawalipi Kodi; kila mtu analipa Kodi indirectly na kutokana na vyanzo vyetu na Tozo tunaweza kuendesha nchi hata bila Kodi ya Mapato; Nikitoa Scenario moja tu ya Makusanyo ambayo mtu analimwa; Kila ukitoa Pesa kwenye Simu, Serikali Inakula, Wakala akipata faida yake Serikali inakula; Kampuni kwenye faida yake Serikali inakula..., na kwa kula kwote huku hakuna value for money inayopatikana..., Kila halmashauri kuna makusanyo yanafanyika ya hapa na pale..., bado kuna VAT huku na kule zinakusanywa kwa asilimia 18 kule unaponunua bidhaa au kulipia huduma.

Kwa makusanyo yote hayo ni nini kinafanyika ? Huduma gani hizo zinafanyika ukizingatia sasa hivi kila kitu kinabinafsishwa na Matumizi ya Serikali yamepungua, kama ni Hospitali kuna BIMA tunalipia, Kama ni Shule na Elimu tunalipia na hata Elimu ya Juu ni Mikopo wala sio Grant....

Kwahio utaona kwamba kuna pesa Nyingi sana inaliwa na hata tukikusanya vipi itaendelea kuliwa..

Nchi ambazo hazina Kodi ya Mapato

Antigua and Barbuda:
Kisiwa ambacho ni kivutio cha watalii (nadhani hata sisi tuna vivutio vya kutosha)
Saint Kitts and Nevis: Vivutio vya Watalii
Bahrain:
United Arab Emirates
: Mafuta
The Bahamas: Utalii
Bermuda: Utalii
The Cayman Islands: Utalii
Vanatu: Utalii
Monaco: Tourism na Banking
Saudi Arabia: Mafuta
British Virgin Islands: Utalii
Brunei:
Kuwait:
Mafuta
Qatar: Mafuta

Hitimisho:
Tanzania tuna vyanzo vingi na kila mtu anaponunua kitu (consume) analipa Kodi, vilevile ukiongezea Utalii, Madini na kila siku tunatembeza bakuli..., Kama tumeshindwa kufanya vitu vya maana kwa kutumia hizo pesa sidhani kama tatizo ni makusanyo bali ni ufujaji....
 
Back
Top Bottom