Mzee Mwanakijiji umekamata kwenyewe.Nadhani Mh.km amerudi ktk hii safu basi hii aiwekee note,ni extract muhimu.Serikali hadi leo bado wapo wanjisuasua kwa copywrites za wasanii tuu hawajui hata ktk patent kunaweza watoa wabongo kibao,kwani mtu km analowazo jipya na zuri akilewekewa patent analiuza au kukopea nalo na kuweza fanya kazi kwa kipindi fulani ambacho atakuwa amerudisha gharama zake na ndio sasa fungulia mbwa ianze ili kuleta upinzani.
Lakini leo hii hata jamaa wa chai maharage enzi zile,au chakula cha waathirika Arusha,Au mchoraji wa leo anaweza fikisha proposal yake bank leo ya kuomba mkopo kwa ajili ya wazo lake kesho akakuta hilo wazo limeshafanyiwa kazi na tajiri moja nguvu za kutisha.
Mzee mwanakijiji hii itapiga bao si utalii peke yake bali kila sector.Patakuwepo mfumuko wa mawazo na ubunifu wa kila nyanja ambao utaleta mafanikio makubwa.Mtaji wa kila raia utakuwa akili yake,na mafanikio ya makampuni yatakuwa mitaji yao.