Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,621
- 8,411
Mwanamuziki mashuhuri kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amekamatwa akiwa nyumbani kwake mjini Kinshasa.
Mwanamuziki huyo amekamatwa kwa agizo la afisi ya mwendesha mashtaka.
Olomide alitimuliwa kutoka nchini Kenya baada ya video kuonekana kuonesha akimpiga teke mchezaji ngoma wa kike katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta mapema asubuhi baada yake kuwasili.
Alipangiwa kutumbuiza mashabiki wake Bomas of Kenya siku ya Jumamosi lakini tamasha hiyo ikaahirishwa.
Alikamatwa Ijumaa usiku na maafisa wa polisi wa Kenya na siku iliyofuata asubuhi akaingizwa kwenye ndege na kurejeshwa Kinshasa.