Koffi Olomide akamatwa DR Congo

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411


Mwanamuziki mashuhuri kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amekamatwa akiwa nyumbani kwake mjini Kinshasa.
Mwanamuziki huyo amekamatwa kwa agizo la afisi ya mwendesha mashtaka.

Olomide alitimuliwa kutoka nchini Kenya baada ya video kuonekana kuonesha akimpiga teke mchezaji ngoma wa kike katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta mapema asubuhi baada yake kuwasili.



Alipangiwa kutumbuiza mashabiki wake Bomas of Kenya siku ya Jumamosi lakini tamasha hiyo ikaahirishwa.

Alikamatwa Ijumaa usiku na maafisa wa polisi wa Kenya na siku iliyofuata asubuhi akaingizwa kwenye ndege na kurejeshwa Kinshasa.
 
Safi sana.. Kidogo wamuadabishe , alichofanya ni kitendo cha udhalilishaji na uvunjaji wa haki ulio wazi wazi.. Haijalishi kama mkata mauno ndo mwenye makosa ila koffi kazingua...
 
Anakamatwa kwa sababu ni maarufu tu, huku mitaani watu wanapiga wake zao kama mabondia na hakuna chochote, Ila kile kiteke cha koffi kinaonekana nongwa, umaarufu wake umemponza!
Wewe hujui watu maarufu ni kioo cha jamii..?
 
Kuna rais alishawahi kuamuru huyu jamaa atandikwe viboko hadharani nafikiri hili lilifanyika

Sasa kwa ishu ya sasa ujue keshakosea masharti ya mganga asipojirekebisha haraka atazisoma tarakimu za namba [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
angepigwa mwanaume sidhani kama yangetokea haya yote, usawa wa me na ke hautatokea
 
Amekamatwa lini mbona yupo Paris na ameomba radhi kwa hlo japo amesema hakua amekusudia
 

Attachments

  • 1469523895775.jpg
    95.2 KB · Views: 53
Safi sana.. Kidogo wamuadabishe , alichofanya ni kitendo cha udhalilishaji na uvunjaji wa haki ulio wazi wazi.. Haijalishi kama mkata mauno ndo mwenye makosa ila koffi kazingua...
Hii ni haki yake na lazima ajifunze ustaarabu, ule ubabe wa usio na tija wenzake waliacha zamaani yeye ndio leo anaufanya. Tena hiyo zamani hawakupigwa wanawake unatafuta mbabe mwenzio halafu unalianzisha, eti yeye anapigana na mwanamke!!? Ndio tumuone mbabe!!!?? Kupitia fursa hii ningewaomba wale waliotaka kumualika huyu jamaa waachane nae (Efm?!).
 
Liwe funzo kwa wote wanaodhani pesa ndio kila kitu, dharau na kiburi ni shimo la mafanikio, avune alichopanda,
 
huyo mzee bora kazoea na hiyo tabia yake wacha wamnyooshe tu ajifunze
 
Kweli kabisa, kama kenya wamemkazia, kongo wamemkazi niliskia na zambia wamekaza, sisi watanzania tutajichoresha tu
 
Hakuna kesi hapo yule dansa keshasema hakubutuliwa
 
Amekamatwa lini mbona yupo Paris na ameomba radhi kwa hlo japo amesema hakua amekusudia

Labda Paris ya Tandahimba Mkuu ila Koffi Olomide amekamatwa kweli. Tusaidie tu kutuulizia kwa huyo aliyekuhabarisha kuwa yupo Paris ipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…