Koffi Olomide akamatwa na polisi, tayari kurudishwa kwao

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Kufuatia tukio la jana lililonaswa na kamera akimpiga teke mmoja wa madensa wake alioandamana nao kwenye tamasha la muziki, hatimaye Koffi Olomide akamatwa na polisi.

Koffi alikamatwa na polisi nje ya studio za Citizen Tv, na kupelekwa uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta tayari kurudishwa kwao, show yake ilikuwa ifanyike leo jumamosi.

Chanzo.. Citizen
 
Duh....inaonekana black belt yake aliipata kimagumashi maana moja ya nguzo ya martial arts ni nidhamu ya hali ya juu na kutopenda kuonea wanyonge bali kuwatetea. Alichofanya kutumia nguvu zaidi dhidi ya mwanamke ni ukiukwaji wa misingi ya marital arts...
 
Koffi Olomide safi akajifunze kuheshimu wanawake mpuuzi sana
 
Nilishangaa sana Mwanaume mzima na ndevu zake nyeupe anamtwanga teke mwanadada asiyekuwa na ubavu wa kupigana naye.
 
Duh....inaonekana black belt yake aliipata kimagumashi maana moja ya nguzo ya martial arts ni nidhamu ya hali ya juu na kutopenda kuonea wanyonge bali kuwatetea. Alichofanya kutumia nguvu zaidi dhidi ya mwanamke ni ukiukwaji wa misingi ya marital arts...
Kama takosea basi nisahihishwe, mwenye black belt ni Werrason
 
Safi Sana na wale askari waliokuwepo pale wafukuzwe kazi walimwacha tu hivi hivi wakati alitenda kosa waziwazi.
 
Safi kabisa hii maana nilishangaa jana wale mapolisi pale uwanjan kuna mmoja alikuwa anamplease jamaa kama yeye ndo katendewa kosa..
 
1469266791904.jpg

Kawa mnyonge ghafla bila kutarajia..!
 
Kufuatia tukio la jana lililonaswa na kamera akimpiga teke mmoja wa madensa wake alioandamana nao kwenye tamasha la muziki, hatimaye Koffi Olomide akamatwa na polisi.
Koffi alikamatwa na polisi nje ya studio za Citizen Tv, na kupelekwa uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta tayari kurudishwa kwao, show yake ilikuwa ifanyike leo jumamosi.

Chanzo.. Citizen

Hata hivyo kwa HABARI za uhakika kabisa zinasema kwamba siyo kweli kama Koffi Charles Antoine Olomide hakufanya hicho Kitendo isipokuwa kilichofanyika ni kitu cha kupangwa kilichofanywa na MAADUI wa Koffi waliomtumia Dancer mmoja wa Koffi aliyefukuzwa Kundini muda mrefu anaitwa Millie a.k.a Neymar ambaye walijua kuwa Jana Koffi Olomide angetua kwa ajili ya Show jijini Nairobi hivyo walichokifanya ni kutengeza MBINU chafu kupitia kwa Watumishi wa Uwanja wa Ndege na Media baadhi kisha wakati Koffi na entourage yake yote wanashuka kutoka katika Ndege Koffi yeye akawa anawahi kwenda kuzungumza na Waandishi wa Habari akiwa ameongozana na Muimbaji na Mtunzi wake Mwandamizi Bouro Mpela Gecco na huku nyuma Mkewe na ambaye pia ni Muimbaji wake Cindy yeye akabaki na wale Dancers kufuatilia mizigo ya Bendi ndipo yule Dada akatoka alikotoka na kwenda moja kwa moja walipokuwa wale Wacheza Show ( Dancers ) wa Koffi na akaanza kuwatukana ndipo mmoja wa Dancers wa Koffi aitwae Nadine Mundele nae akawa anamjibu na hatimaye Cindy nae akaingilia kati ndipo Mlinzi wa Koffi aitwae Marcel akamtaarifu Koffi kuwa kuna tatizo na Koffi mara moja akaachana na yale mahojiano na Press na kuwahi kwenda eneo la tukio na alipofika tu alichokifanya ni kuingilia kati na kuwasihi wale Dancers wake na Mkewe Cindy kuwa waachane nae yule Dancer " mkorofi " na waondoke na hakumpiga Mtu yoyote.

Na ili kulithibitisha hilo muda mfupi tu Koffi Olomide ameitisha Press Conference na ili muone kuwa Media za Kenya baadhi zilitumika kupotosha ni kwamba yule Dada ambaye wao walidai amepigwa teke na Koffi yeye mwenyewe ndiyo ameeleza ukweli, huku Cindy na baadhi ya Askari wa Usalama wa Uwanja wa Ndege waliokuwepo pale jana na wao wameipinga hiyo taarifa kuwa Koffi Olomide amempiga teke Mnenguaje wake.

Kitendo hiki kimemsikitisha sana Koffi Olomide ambapo imembidi sasa aandike ujumbe wake katika Mitandao ya Kijamii mbalimbali kwanza kuwataka radhi WANAWAKE wote na hasa wale ambao WALIPOTOSHWA na hii TAARIFA na kwamba sasa anajipanga KUWASHTAKI wale wote waliotekeleza huu mpango kwa kiukweli hili TUKIO limemchafua mno na sana.

Ni hayo tu Ndugu zanguni na naomba niishie tu hapa tafadhali.
 
Unajua wewe tunakuheshimu,unashindwa na MSAGA SUMU, au kuna mtu ame hack account yako na wewe?
 
Ningeshangaa kama wangemwachia kuendelea na show..! kwa tukio lake
 
Ndio maana meusi yanatwangwa risasi na polisi huko Ulaya na Marekani. Sometimes tunashindwa kujiheshimu; kwa hadhi yake hakupaswa kufanya kitu kama kile hadharani hata kama huyo mdada alifanya kosa la namna gani. Bado ngozi nyeusi inasumbuliwa sana na ujinga, kutojielewa, kutojiheshimu, na hata kuheshimu wengine. Jinga kweli hilo.
 
Back
Top Bottom