Tengu mwana
Member
- Mar 1, 2015
- 35
- 5
Ahahahah! Black belt
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kazi sio kigezo cha kunyanyaswa, atamfukuza kazi na atamlipa stahiki zake maisha yatasonga. Kumbuka wizara husika Kenya itawasiliana na wizara ya Congo na haki itachukua mkondo wake.bahati mbaya huyo binti atafukuzwa kazi na koffiii mwenyewe
Mabosi wanyanyasaji hawa hata hapa bongo wapo mkuu.Nilishangaa sana Mwanaume mzima na ndevu zake nyeupe anamtwanga teke mwanadada asiyekuwa na ubavu wa kupigana naye.
....na Aurusi MabeleKama takosea basi nisahihishwe, mwenye black belt ni Werrason
Mkuu nimeshanga hata uwanja wa ndege wa Ndjili Kinshasa amezomewa.amejiharibia jina. kitu cha kwanza koffi is a convict, ashawahi fungwa miezi mitatu kwa kumpiga producer wake, alafu pia akiwa france alishawahi kuwa accused of raping 3 of his dancers na ku fungia mwengine kwa chumba,.... mtu ukifatwa fatwa na mambo kama haya, lazma kuna ukweli, kwahivyo its not far fetched
amejiharibia sifa zengine, stori imeshasambaa kwa forum na blogsites za kiafrica. soma comments kwa hii site
Koffi Olomide Deported from Kenya after Assaulting a woman at the Airport | Watch
Mkuu nimeshanga hata uwanja wa ndege wa Ndjili Kinshasa amezomewa.
Hii ni dalili ya kuwa watu wamekerwa na lile tukio.. na kama ulivyodokeza baadhi ya matukio, sasa kwanini basi hajitambui..!?
Na lile teke ndo vipi yan..??Hata hivyo kwa HABARI za uhakika kabisa zinasema kwamba siyo kweli kama Koffi Charles Antoine Olomide hakufanya hicho Kitendo isipokuwa kilichofanyika ni kitu cha kupangwa kilichofanywa na MAADUI wa Koffi waliomtumia Dancer mmoja wa Koffi aliyefukuzwa Kundini muda mrefu anaitwa Millie a.k.a Neymar ambaye walijua kuwa Jana Koffi Olomide angetua kwa ajili ya Show jijini Nairobi hivyo walichokifanya ni kutengeza MBINU chafu kupitia kwa Watumishi wa Uwanja wa Ndege na Media baadhi kisha wakati Koffi na entourage yake yote wanashuka kutoka katika Ndege Koffi yeye akawa anawahi kwenda kuzungumza na Waandishi wa Habari akiwa ameongozana na Muimbaji na Mtunzi wake Mwandamizi Bouro Mpela Gecco na huku nyuma Mkewe na ambaye pia ni Muimbaji wake Cindy yeye akabaki na wale Dancers kufuatilia mizigo ya Bendi ndipo yule Dada akatoka alikotoka na kwenda moja kwa moja walipokuwa wale Wacheza Show ( Dancers ) wa Koffi na akaanza kuwatukana ndipo mmoja wa Dancers wa Koffi aitwae Nadine Mundele nae akawa anamjibu na hatimaye Cindy nae akaingilia kati ndipo Mlinzi wa Koffi aitwae Marcel akamtaarifu Koffi kuwa kuna tatizo na Koffi mara moja akaachana na yale mahojiano na Press na kuwahi kwenda eneo la tukio na alipofika tu alichokifanya ni kuingilia kati na kuwasihi wale Dancers wake na Mkewe Cindy kuwa waachane nae yule Dancer " mkorofi " na waondoke na hakumpiga Mtu yoyote.
Na ili kulithibitisha hilo muda mfupi tu Koffi Olomide ameitisha Press Conference na ili muone kuwa Media za Kenya baadhi zilitumika kupotosha ni kwamba yule Dada ambaye wao walidai amepigwa teke na Koffi yeye mwenyewe ndiyo ameeleza ukweli, huku Cindy na baadhi ya Askari wa Usalama wa Uwanja wa Ndege waliokuwepo pale jana na wao wameipinga hiyo taarifa kuwa Koffi Olomide amempiga teke Mnenguaje wake.
Kitendo hiki kimemsikitisha sana Koffi Olomide ambapo imembidi sasa aandike ujumbe wake katika Mitandao ya Kijamii mbalimbali kwanza kuwataka radhi WANAWAKE wote na hasa wale ambao WALIPOTOSHWA na hii TAARIFA na kwamba sasa anajipanga KUWASHTAKI wale wote waliotekeleza huu mpango kwa kiukweli hili TUKIO limemchafua mno na sana.
Ni hayo tu Ndugu zanguni na naomba niishie tu hapa tafadhali.