Koffi Olomide azidi kukinukisha mbaya

Koffi Olomide azidi kukinukisha mbaya

Sodium 23

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2013
Posts
483
Reaction score
491
Habari zenu wanajukwaa! Bila shaka mu wazima wa afya.
Mwaka huu umekua hauna likizo kabisa kutokana na Kamanda Koffi Olomide Mopao Mokonzi Quadra Korea Man aka Le Treisième apôtre kuachia album mpya ya Nyataquance ambayo inasumbua dunia mwaka huu.

Kama kawa alianza na Nyataquance yenyewe tukanyata nayo kwa miezi kadhaa lakini punde si punde akaachia Alidor na diaspora special kwa Didi Stone (binti yake anayeishi Marekani kama sikosei).
Kabla hatujapumzika kaachia kitu cha Tshou Tshou Tshou almaarufu kama kalembelembe ambayo imesumbua kuanzia Club hadi vibanda umiza. Kilichonivutia kwenye Tshou tshou tshou ni chorus na staili ya kucheza Allez dance ya ba boss.

Nyataquance na Tshou tshou tshou zilikua na surprise ya sauti mpya ya Kirikou tofauti na wengi tulivyotarajia kusikia sauti ya Cindy le coeur.
Na kama hiyo haitoshi tarehe 1 October kaachia mzigo mpya Charisma ambayo umeshaanza kupigwa maeneo mengi mjini.
Mwaka huu ni hatari kwa upande wa burudaniiiiiiiiii.
Nawatakia wakati mwema wakuu.
 
Kusema ukweli jamaa anajua.
Namkubali sana kwenye bolingo za taratibu
 
Kalembelembe[emoji444] [emoji445] [emoji444]
 
Koffi olomide ni msanii wangu No. 1 duniani huyu mtu ni fundi wa ajabu katika hisia zangu za kimaisha, Nina playlist ya Koffi ngoma kama 40+
Haki ya mungu kuna watu unaweza tamani wasife hapa duniani Mmoja wapo ni Koffi Olomide na Cristiano Ronaldo
 
Kuna sehem nimemsikia akitaja jina 'Jack Pemba' ktk hiyo ngoma Charisme ni huyu huyu jamaa aliesumbua miaka fulani hapa bongo na nasikia anaishi Uganda kwa sasa au sijasikia vzr tu hapo
 
Koffi olomide ni msanii wangu No. 1 duniani huyu mtu ni fundi wa ajabu katika hisia zangu za kimaisha, Nina playlist ya Koffi ngoma kama 40+
Haki ya mungu kuna watu unaweza tamani wasife hapa duniani Mmoja wapo ni Koffi Olomide na Cristiano Ronaldo
Ni ukweli kabisaa
 
Back
Top Bottom