Koffi Olomide ndio msanii bora wa muda wote kutoka Congo

Magie ilitoka nadhan1992, na 1994 ni albamu ya V12 ikiwa na wimbo kama Andrada.
Kiujumla Koffi Olomide kadumu sana kwenye muziki akiwa juu, albamu zake kama Loi, Rondpoint aliyowadis Zaiko, Attetant, Force de Frape, Effrakataa, Affaire de etate(kwangu mm ndiyo albamu bora ya muda wote ya Koffi inanyimbo kali sana), Monde arabe (2nd best albam) na Danger de Mort.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Luambo ni 2nd generation na Koffi ni 3rd Generation ya Music wa Congo, hapo vionjo lazima viwe tofauti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tuweke record sawa, Ferre gola hajatolewa na Koffi, Fere ni zao la Werrason. Ferre ameenda QLI akiwa tayari na heshim yake nzuri tu kuliko fally... nyumbo kama Vita Imana tayari zilikuwa zimeshamfanya imjue Herve ni nani...
 
tuweke record sawa, Ferre gola hajatolewa na Koffi, Fere ni zao la Werrason. Ferre ameenda QLI akiwa tayari na heshim yake nzuri tu kuliko fally... nyumbo kama Vita Imana tayari zilikuwa zimeshamfanya imjue Herve ni nani...
Tuweke sawa record Mkuu, Ferre Gola ni zao la Wenge Musica na sio Werrason.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
uko sahihi zaidi mkuu. nashangaa mtu anaposema Fere ni zao la Koffi.
Tuweke sawa record Mkuu, Ferre Gola ni zao la Wenge Musica na sio Werrason.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Hapana si kweli kabisa huyu hata Pepe Kalle hamkuti kabisa kabiaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kweli koffi olomide papa fololo hana mpinzani.hao kina franco,pepe kale,papa wemba hawamfikii kidogo labda kama utakua umeamua kubisha.kipaji cha koffi toka dunia iumbwe hakuna aliyekifikia kwa upande wa sekta yake.ultimutum ni moja ya nyimbo bora,akadabra,tsou tsou,selfie aisee huyu jaamaa aishi miaka mingi kila nyimbo yake kali nikisema niorodheshe nitakesha.mopao mokonzi,papa mourinyo,quarda kora man namkubali sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
From NOBLESSE OBLIDGE to XXXX.
 
Luambo ni 2nd generation na Koffi ni 3rd Generation ya Music wa Congo, hapo vionjo lazima viwe tofauti

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu afadhali wewe umeliweka hili kwa njia tofauti, lakini kuna mtu humu alimlinganisha Franco-Le Grand Maitre Franco tena akuita mkulima-yaani akimlinganisha na Koffi anaona Franco ni mkulima tu. Haya ni matusi makubwa na ndio nikamjibu hivyo. Wadogo zetu saa nyingine wanazidisha mahaba.
 

Watu watambue kuwa Franco pamoja na kuwa walikuwa na kundi moto vilevile Rais Mobutu Seseseko Wazabanga alimbeba sana katika kumfanya afahamike mataifani. Ukirudi kwa Koffi Olomide nae alipigana sana kusimama kivyake mkumbuke kuwa miaka ya zamani ilikuwa ngumu kwa kijana mdogo usimame peke yako na kutengeneza kikundi cha muziki, na ndo maana ukiangalia sana wanamuziki wengi walikuwa hawampendi Koffi, na yeye alilitambua hilo, hata matamasha yake kadhaa ulaya na Zaire enzi zile yalihujumiwa sana, lakini hakukata tamaa na akasimama na hadi leo anatisha. Koffi Olomide anakubalika sana nje ya Congo
 
Mkuu usitumie nguvu nyingi kubishana na hivi vitoto vya miaka ya 90. Yani mtu anasikiliza masebene ya koffi olomide akiwa bar halafu anadiriki kuja huku na kumfananisha na Franco!?!! Seriously??? HAYA NI MATUSI MABAYA SANA.
Mungu na awasamehe bure.
Koffi olomide ni msanii mkali sana dunia hii lakini kwa Franco haifikii hata 0.000001 level zake ni za kina hao Jb mpiana, sijui ferre Gola na yule mfanyakazi wake wa zamani aitwae Ipupa.
Mtu akiendelea kumdharau Franco namporomoshea matusi mazito sana hadharani.
 
Mkuu naona unamshusha Franco kwa style fulani hivi. Kundi hilo la moto unalo lizungumzia ni kazi halisi ya Francois Luambo na Victor Longomba walilijenga toka chini. Pili Mobutu alikuwa FANATIC wa OK Jazz hapo aliposhika madaraka 1965 Franco na OK Jazz walikuwa wameshajipanga na kufahamika hata nje ya Congo (East, Central and West Africa). Sisi tulicheza sana kitu inaitwa Polo na Bolingo ya Bougie enzi hizo. Mobutu alichofanya kwa sababu alikuwa FANATIC wa Luambo alimwambia tukiwa pamoja utafika mbali.
Sina nia ya kumshusha Koffi hivyo sitamzungumzia sana ninachosema ni hiki hawa "Franco na Koffi" si watu wa kulinganishwa, Franco alikuwa a Musical Genious.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…