De Opera
JF-Expert Member
- May 23, 2013
- 780
- 1,664
Habari za muda huu wanaJF? Natumaini mnaendelea vizuri.
Huwa kuna malalamiko, wananchi kuilaumu serikali miundo mbinu na huduma ni mbovu. Hata mimi ni mmoja wapo kwa baadhi ya mambo lakini jinsi yalivyo off key. Ila mimi ni kwa wahudumu. Kiufupi ni kuwa, baadhi ya watoa huduma hawana ueledi. Wanafanya vitu ki-local sana. (Nukta!)
Nakuja huku mjini sasa kwenye wananchi. Na hapa mimi siilaumu serikali bali ni sisi Wananchi & Watoa kuduma.
Yaani kiukweli tatizo ni baadhi ya sisi wananchi na watoa huduma. Hatuthamini vitu vyetu. Hatujivunii na kuvitunza.
Wananchi tunaharibu, watoa huduma nao wanapuuzia. Labda pengine wanaweza kupuuza kwa sababu ya kila aina ya tabia za wananchi.
Serikali imetengeneza public toilets, mtu anaenda kujisaidia pembeni, au hamwagi maji, au anaburuza matako ukutani, au anang'oa koki za maji anaondoka nazo. 😢
Mfano tu utaona jinsi hali ilivyo katika maeneo mbalimbali kama viwanja vya mpira, masoko, na hospitali.
Serikali imeweka vibao vya mitaa, wananchi tunang'oa. Wakati mwingine unakutana na nguzo tu, bati halipo. Ama unakuta limekunjwa kunjwa hadi chini.
Tukiingia kwenye usafiri wa umma, mikono yetu haiwezi kutulia. Tunachokonoa na kuharibu chochote kilicho mbele yetu.
Barabara ni zetu, lakini unakuta mtu anaburuza vyuma huku amefunga nyuma ya usafiri. Mwisho wa siku barabara ikiwa mbovu lawama ni kwa serikali.
Iwe vituo/stendi zote. Mtu badala ya kukaa apumuzike au angojee usafiri, yeye anaanza kukwangua rangi ya ukuta. 😢
Wahudumu wa kwenye huduma za kiserikali serikali nao baadhi hawana akili timamu (zero brain, zero perception kabisa). Hawana uwezo wa ku-percept watu. Wao ni Kujibu watu vibaya, kuwafokea. Kujiona kama wao ndio wameyapatia. Sasa hii kolabo ndio inasababisha lawama kwa serikali , na hii changamoto isipoisha na malalamiko hayawezi kuisha.
Ahsanteni!