Kolo Muani na Kylian Mbappe watimiza matakwa ya mizimu ya babu zao waliolala Cameroon na Congo

Kolo Muani na Kylian Mbappe watimiza matakwa ya mizimu ya babu zao waliolala Cameroon na Congo

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
Jana mchana niliposema Waafrika tulimtuma Kolo Muani kuwapiga kibao Morocco kwa kusema wao sio waafrika na leo tunamtuma Kylian Mbappe kuwapiga ngumi Argentina ilionekana ni kama jambo jepesi lakini lilibeba maana nzito ya kiulimwengu! Waargentina waliwatesa Waafrika miaka ya 1870 hadi 1900 na Waafrika walipotea kabisa nchini Argentina,Mababu zetu walioshuhudia utumwa na unyanyasaji walimtuma Kylian Mbappe kuwaadhibu Argentina na kwa hakika ngumi alizowapiga ziliwapata na maumivu waliyasikia,shukrani kwa Shujaa Kylian Mbappe,umetimiza matakwa ya Mababu zetu,magoli yako yaliiteka dunia na kuifanya dunia nzima iwaze kwa pamoja,

Kwa muda mmoja na jicho la pamoja,Si jambo jepesi hata kidogo!Uamuzi wa nguvu muda katika mambo makubwa hutumika mataifa makubwa katika matukio makubwa kiroho mfano;masaa ya kuanzisha vita huzingatia sana muda,tarehe ya kutangaza kiongozi mkubwa ni muda, masaa ya kuzika kiongozi mkubwa ni muda na mambo mengi ya kutafta ushindi kwa msaada wa nguvu za kiroho! kila Mbappe alipofunga Waargentina waliinama chini kwa majonzi na maumivu,Mababu zetu walifurahi,niliweza kuwaona kwenye uso wa Kylian Mbappe,ahsanteni mababu zetu mlio na nguvu katika Ulimwengu wa roho,asilimia 70% ya watu duniani jana kwa wakati mmoja! waliona Argentina wakipigwa na Kylian Mbappe,hadi jana mchana katika ulimwengu wa kiroho ilishatokea na ilikuwa haibadilishiki hadi mechi iishe.

-Kylian Mbappe apokea kijiti cha Mchezaji bora wa dunia toka kwa Lionel Messi.

Fainali ya Kombe la dunia Qatar 2022 ilikuwa ni ya kupokezana kijiti kwa wachezaji bora wawili Lionel Messi na Kylian Mbappe kwa kiluguru tunasema "passing of the torch" Kylian Mbappe anachukua kijiti toka kwa Christian Ronaldo na Lionel Messi,kwa "hat tricky" ya Kylian Mbappe kwenye fainali ya Kombe,kwa kisukuma wanasema "in the grandest stage of them all" tayari Kylian Mbappe anamuacha mbali Neymar,fainali ya Jana imemfanya Kylian Mbappe kuwa bora zaidi ya Neymar,angalia goli la pili la Ufaransa,pasi maridadi toka kwa Kingsley Coman inafika mguuni kwa Kylian Mbappe,speed ya maamuzi katika ubongo uliotafsiri vizuri Carbohydrate hadi kwenye miguu ya Mbappe inabadili mchezo na matokeo yanasomeka Argentina 2-2 Ufaransa,Mshambuliaji namba kumi wa dunia akifanya mavituzi si hata Pele ambae aliingia kama sub katika mechi ya Kombe la dunia akiwa na umri kama wa Kylian Mbappe.

Uwezo wa Mbappe kufanya maamuzi,pace yake, dribbling vinamfanya Mbappe kuwa wa kipekee katika kundi la wachezaji bora wa dunia kuwahi kutokea,Uwezo wa Mbappe kumiliki mpira,uwezo wake wa kufikiri na uwezo wake wa kufanya maamuzi ni sahihi kwa 9/10 ambayo inamfanya kuwa Mchezaji wa thamani kubwa linapokuja suala la kutumia mpira,hakuna kupotea kwa mpira wala kukosa goli pale kwenye uhitaji, Wachezaji kama Messi, Ronaldo,Neymar,Rooney,Zidane,ni wazuri kwenye kupiga pasi lakini issue sio kupiga pasi bali maamuzi ndio kitu muhimu,uamuzi wa kupiga pasi hadi anayekukaba anajiuliza imewezekana vipi,amewezaje kupiga pasi,spidi ya maamuzi ya Mchezaji kama Kylian Mbappe ni muhimu sana katika kubadili mchezo kama ilivyokuwa kwenye fainali ya Jana,

Nimalizie na neno "spidi ya mpira" ambayo wachezaji wengi wa Tanzania hawana na wanapaswa kufanyia zoezi eneo hilo,Spidi ninayozungumzia ni "kufanya maamuzi" kwa kihaya wanaita "decision making" wapo Wachezaji wachache kama Clatious Chama kwa hapa Tanzania,na kwa dunia yupo Kylian Mbappe,wapo wengine kama Theo Walcott ambae anaweza kukimbia na mpira lakini katika maamuzi ya nini cha kufanya ninapokimbia au kupiga mpira hawamfikii Kylian Mbappe,pengine Xavi anaweza kuwa kwenye kundi moja na Mbappe,ball control na maamuzi, lazima kujua unapokuwa na mpira ndio hatari inakusubiri mbeleni kwa hiyo maamuzi ya nini kinafuata ndio kitu muhimu.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the effect of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
1671388727811.jpg



The man who stolen the show japo hajafunga ila balaa lake mmeona..We endelea kuangalia ngozi nyeusi .
 
Kipindi Cha pili kocha alitoa wazungu wote akaweka waswahili tupu kasoro kipa
 
-Kylian Mbappe apokea kijiti cha Mchezaji bora wa dunia toka kwa Lionel Messi.
NO mbappe ni mfungaji bora wa mashindano ya kombe la dunia but
KING KING KING LIONEL ANDRES MESS
Ndie mchezaji Bora wa kombe la dunia.
 
Back
Top Bottom